WAFAHAMU WATANZANIA WAWILI MIONGONI MWA WANACHAMA MASHUHURI WANNE WA BODI YA USHAURI YA KIDIPLOMASIA YA AFYA YA JAMII YA KIMATAIFA

MUUNGANO   MEDIA
0


 
Dkt. Julietha Tibyesiga, Mtetezi na Muelimishaji wa Afya ya Uzazi Kwa vijana rika balehe


Dkt. Ntuli Kapologwe, Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA-HC)



Wanachama Wanne Mashuhuri wa Bodi ya Ushauri ya Kidiplomasia ya Afya ya Jamii ya Kimataifa


Watanzania wawili wamepata fursa ya kuwa miongoni mwa wanachama Mashuhuri wane wa Bodi ya Ushauri ya Kidiplomasia ya Afya ya Jamii ya Kimataifa(International Health Diplomacy Advisory Group)

Miongoni mwa wanachama wanne mashuhuri wa bodi hii kutoka Tanzania ni Dkt. Ntuli Kapologwe, Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA-HC) ambaye pia aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya ,pamoja na Dkt. Julietha Tibyesiga, Mtetezi na Muelimishaji wa Afya ya Uzazi Kwa vijana rika balehe, ambaye kwa sasa anajitolea katika Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma chini ya Idara ya Huduma za Kinga, Wizara ya Afya.

Ushiriki wao unaakisi dhamira thabiti ya kukuza sauti na uongozi wa Kiafrika katika kuunda mustakabali wa kidiplomasia ya afya.
Wanachama wengine wa bodi ya Ushauri ya Kidiplomasia ya Afya ya Jamii ya Kimataifa ni pamoja na Dkt. Janilza Silva kutoka nchini Cabo Verde na Dkt. Luis de Almeida Sampaio kutoka nchini Ureno.

Ikumbukwe kuwa, Bodi ya Ushauri ya Kidiplomasia ya Afya ya Jamii ya Kimataifa, imeanzishwa mwaka huu chini ya Shule ya Afya ya Umma ya Chuo Kikuu cha Memphis nchini Marekani, inahudumu kama jukwaa la kimkakati linalowakutanisha wataalamu wakuu katika afya ya kimataifa, uhusiano wa kimataifa, na sera za umma. Bodi hii ya ushauri yenye taaluma mbalimbali imejikita katika kuimarisha nyanja ya Kidiplomasia ya Afya, eneo muhimu linalounganisha afya ya jamii na ushirikiano wa kimataifa.

Kuanzishwa kwa Bodi hii inatokana na kutambua kwa kiwango kikubwa hitaji la kuwa na wanadiplomasia wa afya walio na uwezo wa kusimamia majadiliano ya afya ya kimataifa, kukuza usawa, na kuendeleza ushirikiano madhubuti kimataifa. Kutokana kwa ongezeko la magonjwa kuvuka mipaka ya kitaifa, umuhimu wa kuwapatia wataalamu wa afya ya jamii nyenzo za kidiplomasia ni wa dharura sana.

Kazi kuu ya Bodi hii ya Ushauri ni kutoa mwongozo wa kimkakati wa hali ya juu, kukuza ushirikiano wa kimataifa, na kuunga mkono Maabara ya Kidiplomasia ya Afya ya Jamii iliyokwisha anzishwa ,maabara hii ni bunifu ya kuwaandaa wanadiplomasia wa afya watakaoweza kukabiliana na changamoto za afya duniani, hasa katika nchi za kipato cha chini na cha kati.




Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)