SHIRIKA LA SAVE THE CHILDREN NCHINI TANZANIA YATOA ELIMU YA UPANDAJI MITI.

MUUNGANO   MEDIA
0



Katika kuadhimisha  Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Shirika la Save the Children limeshirikiana TFS pamoja na Halmshauri ya Wilaya ya Chamwino Jijini Dodoma kupanda miti ya matunda na Vivuli katika shule ya Sekondari Mwalimu Nyerere.


Hatua hiyo inakuja katika kuendeleza program ya lishe Bora Ili Kila mtoto ajifunze na kujua umuhimu  wa kula Matunda katika kila mlo wake.


Akizungumza baada ya zoezi la upandaji miti Mkuu wa Wilaya ya Chamwino mhe,Janeth Mayanja amesema watanzania wanapaswa kuyaenzi yaliyofanywa na waasisi wa Taifa hili kwa kutunza mazingira,kupanda miti na kuulinda Muungano ili uendelee kuwa Imara.


"Ni wajibu wetu kuulinda na kuutunza Muungano wetu na kuuadhimisha Kwa kufanya usafi,kupanda miti na kuendeleza masuala ya lishe na utamaduni,"Alisema Mayanja.


Kwa Upande wake Mratibu wa Shughuli za kilimo na Ufugaji kutoka Shirika la Save the Children Mwita Charles amesema wamefanikiwa kupanda miti 200 na kutoa elimu ya namna ya kupanda miti ya matunda na namna ya kutunza Ili isikauke ambapo katika shule hiyo wanatarajia kupanda jumla ya  miti 500 ya matunda na kivuli.


Mwita amesema lengo ni Kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya Nchi lakin pia kutoa elimu Kwa  wanafunzi kujua umuhimu wa matunda katika lishe na kuepukana na udumavu.


Aidha,baadhi ya wanafunzi katika shule hiyo wameishukuru Shirika la Save the Children  kwa kutoa elimu ya upandaji wa miti na utunzaji wake maana itawasaidia kupata lishe Bora Kwa Kula matunda na kivuli kwa ajili ya kujisomea wakati wa mapumziko.


Mwisho.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)