MAKATIBU WAKUU WAKUTANA KUJADILI MASUALA YA LISHE.

MUUNGANO   MEDIA
0


Mkurugenzi  Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya Dkt. Ntuli Kapologwe  ameshiriki kikao cha Makatibu Wakuu kwa lengo la kupitia andiko la Lishe kwa ajili ya mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika .


Kikao hicho kimefanyika Tarehe 08, Februari 2024 katika Ukumbi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Jijini Dodoma  ambapo Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Dkt. Wilson Charles Mahela ameongoza kikao hicho.  


Ikumbukwe kuwa Wataalam wa masuala ya Afya wana kauli isemayo ujionavyo ni kutokana na vile unavyokula. Hii ina maana anachokula binadamu au kiumbe hai chochote ndicho huufanya mwili wake uonekane vile ulivyo.


Ni kutokana na hali hiyo wataalamu wa masuala ya lishe wanasisitiza pia umuhimu wa lishe bora kwa watoto kuanzia wakiwa tumboni , baada ya kuzaliwa na kadiri wanavyoendelea kukua hadi kufikia utu uzima na hadi uzeeni.


Wataalamu wa Afya wanaeleza kuwa Lishe bora kwa mtoto ni sehemu ya mambo muhimu matano yanayowezesha ukuaji stahiki wake. Yaani Lishe inaungana na mambo mengine manne ambayo ni pamoja na Malezi yenye muitikio, Afya bora, Ulinzi na Usalama na Ujifunzaji wa awali.


Lakini Lishe isiyo ya Mlo Kamili pia si bora hivyo lazima izingatie vyakula vyenye kuwezesha mlo kamili.Mlo kamili ni mkusanyiko wa vyakula mbalimbali ambavyo kwa pamoja huimarisha na kuujenga mwili wa binadamu na wanyama kwa sababu vinaleta virutubishi vyote vinavyohitajika.


 Kwa watoto wadogo suala la lishe sahihi haliishii tu kwa uandaaji wa vyakula vya mlo kamili bali ratiba iliyo sahihi pia ni muhimu. Ratiba ya ulaji wa mtoto mdogo ni tofauti na ya mtu mzima.

 

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)