WATUMISHI WOTE WANASTAHILI KUHESHIMIWA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 

Akizungumza wakati  akiwasilisha mada kuhusu Mawasiliano ya Kimkakati katika Mafunzo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa Watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania tawi dogo la Dar es Salaam Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini amewataka Viongozi ambao hutumia lugha za kejeli,dharau na udhalilishaji kwa wadogo kuacha tabia hiyo kwani kila Mtumishi anapaswa kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wake.


Naibu Waziri Sagini amesema kuwa  Mawasiliano yenye tija  ndani ya Taasisi, Jamii na Wadau wa Nje na Ndani  ambao Taasisi hiyo  inawahudumia ni mambo ya msingi yanayopaswa kuzingatiwa ili kuifanya Taasisi kufikia malengo yake kwani kila mdau anapenda kupata taarifa sahihi  na kwa wakati sahihi.


"Mawasiliano yazingatie kufanyika kwa staha na itifaki sahihi. Wapo Viongozi ambao hutumia lugha za kejeli,dharau na udhalilishaji kwa wadogo zao jambo hili sio zuri kwani huathiri mawasiliano.Viongozi wa Kisiasa,Watendaji Wakuu na Watumishi waliopo chini wote wanastahili kuheshimiwa na kuthaminiwa utu wao."Alisema Sagini


Kwa upande wake Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Emmanuel Tutuba amesema kuwa Taasisi hiyo imeona ni vyema kuwa na mafunzo ya namna ikiwa ni sehemu ya kuwajengea uwezo na kubadili mwenendo wa utendaji kazi wa Watumishi wake jambo ambalo litasaidia  kuongeza ufanisi na kuiwezesha Benki Kuu ya Tanzania  kufanikisha malengo yake.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)