Angela Msimbira TABORA.
Timu za Mikoa ya Mwanza, Arusha na Shinyanga zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya mchezo wa Netiboli kwenye mashindano ya UMITASHMTA yanayondelea katika viwanja vya shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora.
Katika michezo hiyo iliyochezwa Jumamosi Tarehe 10 Juni 2023, Geita imeifunga Kagera magoli 57-24, Simiyu ikapoteza mbele ya Mwanza kwa magoli 75 - 34 , Arusha ikaifunga Dodoma magoli 46- 32 na Shinyanga ikaiadhibu Pwani Magoli 45-24.
Kwa upande wa Mchezo wa Kikapu wavulana mikoa iliyoingia fainali ni Mwanza, Unguja,Pemba na Dar es Salaam, huku mchezo uliokiwa na ushindani mkali kati ya Mwanza na Shinyanga ukimalizika kwa Mwanza imeibuka kidedea baada ya ushindi wa vikapu 17-12.
Timu ya Kanda ya Unguja iliifunga Mbeya vikapu 82 -42, huku Kanda ya Pemba ikiuondoa mashindanoni Mkoa wa Tanga kwa kipigo cha 50-23 na Dar es salaam kuwafunga wenyeji Tabora kwa vikapu 61-17.
Kwa Upande wa Mpira wa Mikono wavulana Mkoa wa Songwe umewafunga wenyeji Tabora kwa magoli 23-18, Kilimanjaro ikafungwa na Shinyanga 18-19, Dar-es-salaam ikibuka na ushindi dhidi ya Mara kwa magoli 23 -17 kisha Mwanza ikaifunga Rukwa 27-12.
Aidha katika Mpira wa Mkono Wasichana Mkoa wa Geita ulishinda Mara magoli 18-12, Kigoma ikikubali kipigo kutoka Rukwa kwa magoli 14-12, Dar es salaam ikafungwa na Tabora kwa magoli 17 -12, huku Songwe ikifungwa na Morogoro kwa magoli 11-13.

