WANAFUNZI MKOANI KIGOMA WAHAMASIKA KATIKA KILIMO CHA MBOGAMBOGA SHULENI.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na. Elimu ya Afya kwa umma.

Wanafunzi wa shule za Sekondari Kigoma na Buhanda ni miongoni mwa shule zinazofanya vizuri katika kilimo cha bustani za mbogamboga na matunda, hivyo kuchangia katika kuongeza upatikanaji na utumiaji wa chakula shuleni.

Hayo, yamebainishwa na Ofisa Lishe wa Manispaa ya Kigoma, Bw. Omari Kibwana wakati akitoa mrejesho wa huduma ya chakula na Lishe shuleni katika Manispaa hiyo, mnamo tarehe 11 Mei, 2023.

Halikadhalika Bw. Omari alibainisha kuwa uhamasishaji wa kilimo cha mbogamboga na matunda ni utekelezaji wa agizo la Serikali kupitia Mwongozo wake unaoelekeza utoaji wa huduma ya Chakula na Lishe kwa wanafunzi wa shule zote za elimu ya msingi hadi kidato cha nne husani shule za kutwa.

Kwa Upande wake Bw. Mengo Chikoma; Ofisa Mradi wa Kuhamasisha Kilimo cha bustani za mbogamboga, matunda na lishe bora kutoka Shirika lisilo la Kiserikali la ANUE amebainisha kuwa; shule hizo wameziteua kuwa shule za mfano wa kuigwa kwa shule zingine na jamii kujifunza kuhusiana na kilimo cha mbogamboga na matunda.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)