Wiki nne zimepita tangu vilipoanza vita kati ya jeshi sudan na vikosi vya msaada wa haraka. Athari mbaya za kiuchumi za vita hivyo zinazidi kuonekana kwenye uchumi wa nchi jirani, hasa zile ambazo masoko yake yanatemea sana bidhaa zinazopitia nchini Sudan.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim, Sudan inapakana na nchi saba za Afrika na inauza nje bidhaa kama vile nyama, nafaka na bidhaa nyingi za chakula kwa majirani wake wengi. Lakini vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyozuka nchini Sudan hivi sasa vimesababisha zaidi ya bidhaa 90 za nchi hiyo kutofika tena nchi jirani.
Kwa mujibu wa gazeti la Al-Mashad al-Sudani linalochapishwa mjini Khartoum, asilimia 70 ya soko la bidhaa za chakula nchini Sudan Kusini na Jamhuri ya Afrika ya Kati hutegemea bidhaa za Sudan kama vile sukari, unga, nyama, nyanya, mafuta ya kula n.k. Pia, asilimia 30 hadi 60 ya soko la Misri linategemea mazao ya kilimo na mifugo ya Sudan.
Chanzo #Parstoday.
.
