TANESCO HATUUZI NGUZO BALI TUNATOA HUDUMA YA UMEME.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi wa huduma kwa wateja kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Martin Mwambene amesema kuwa shirika hilo haliuzi nguzo bali linauza huduma ya umeme.

Mwambene ameyasema hayo leo Februari 22,2023Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu majukumu na utekelezaji wa shirika hilo.

Amesema TANESCO) inatekeleza miradi kadhaa ya kuzalisha umeme ambayo itasaidia kuongeza kiwango cha umeme katika Gridi ya Taifa kila mwaka huku likiwa na lengo la kuzalisha Megawati 5000 hadi 6000 ifikapo 2025 na kuuza nje ya nchi.

“Kwasasa Mradi wa Umeme wa bwawa la Julius Nyerere upo asilimia 88 ambapo sasa hivi tumeanza kujaza maji ambayo yamefikia mita za ujazo 133 kutoka usawa wa bahari.

“Najua Wateja wamekua wakijiuliza TANESCO hawafikirii kutafuta njia mbadala lakini sisi kama TANESCO tumefikiria kuwa na mbinu za miradi mbadala ambayo itaongeza uwezo wa uzalishaji wa umeme ikiwemo ya gesi na jua, pia kuna vyanzo binafsi vyenye uwezo wa kuzalisha umeme mfano viwanda vya sukari,”amesema.



Aidha amesema kuwa Miradi ya uzalishaji umeme inaenda sambamba na miradi ya kusafirisha umeme, katika mradi wa JNHPP ambapo kuna njia ya kusafirisha umeme itakayoanzia Rufiji mpaka Chalinze na tayari transfoma kubwa takriban sita zimepelekwa zinasubiri kufungwa.

“Kuna baadhi ya mikoa ikiwemo Rukwa na Katavi haipo katika Gridi ya Taifa, hivyo kuna laini ambazo zitajengwa ambazo zitakuwa zinaunganisha nchi na nchi nyingine karibu nchi nzima itakuwa ipo katika mfumo wa Gridi ya Taifa,”amefafanua.

Mwambene ameeleza kuwa utatekelezwa mradi wa Gridi Imara utajumuisha ununuzi wa mashine umba 6,000, mita laki 7 za umeme, nguzo 380,000, ununuzi na ufungaji wa nyaya zenye urefu wa KM 40,000, ujenzi wa vituo 14 vya kupoza umeme na ujenzi wa njia za kusafirisha umeme mkubwa takriban KM 948.

“Mradi huu wa Gridi Imara ni ushahidi kwamba matatizo ya umeme yaliyopo nchini tunayafahamu na tunatarajia mradi huu utayatatua,”amesema.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)