WANANCHI LUNGUYA MSALALA KAHAMA WALALAMIKIA KWA KITUO CHA AFYA KUKOSA VIFAA MUHIMU NA BADALA YAKE WANANUNUA JIRANI NA KITUO CHA AFYA

1


Wananchi wa kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wamelalamikia kutokana na kituo cha Afya cha Lunguya kukosa vifaa muhimu ikiwa ni pamoja na mipira ya kujifungulia kwa akina mama wajawazito.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wananchi hao wamesema kuwa suala la mipira katika kituo hicho imekuwa changamoto kwao ambapo hununua kwa shilingi elfu 3000  karibu na eneo la kituo hicho.

Aidha wananchi hao wameomba  serikali kuongeza idadi ya watumishi katika kituo hicho kwani kinahudumia wakazi wengi  .

Akijibu hoja hiyo diwani wa kata ya Lunguya  Benedict Manuary amesema kuwa kutozwa mpira wa kujifungulia kwa akina mama wanaojifungua linakwendana kinyume na matakwa ya serikali na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano pindi wanapokumbwa na matatzizo.

Naye mbunge wa jimbo la Msalala amesema kuwa ni vyema kuyaripua mapema mafisadi kabla hayajaota mizizi huku akishangazwa kwa kituo hicho kukosa vipimio vya kupimia magonjwa madogo madogo kama vile malaria .

Chapisha Maoni

1Maoni
  1. WANANCHI NI JAMBO LA BUSARA KUPAMBANA NA MIMBA PAMOJA NA UTOAJI WA MIMBA

    JibuFuta
Chapisha Maoni