ELIMU YA AFYA JUMUISHI KUTOLEWA KWA MAKUNDI MAALUMU MTWARA.

MUUNGANO   MEDIA
0


 Na.Elimu ya Afya.


Timu ya Watalam kutoka Wizara ya Afya, Idara Kinga, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma pamoja na Idara ya Afya Uzazi Mama na Mtoto inewasili Mkaoni Mtwara kwa lengo la kutoa Elimu ya umuhimu wa kuhudhuria kliniki wakati wa ujazito pamoja na kutambua dalili za hatari kwa Mama mjamzito pamoja na watoto wa changa, Elimu kuhusu magonjwa ya mlipuko ikiwemo Mpox, Kipindupindu na Dengue.


Elimu hiyo Jumuishi itatolewa katika Halmshari za Tandahimba na Nanyumbu ikihusisha makundi ya viongozi wa dini, Viongozi wa kimila, Viongozi wa Kimwinyi, Watoa huduma za Afya ngazi ya Jamii , Watoa huduma za Afya katika vituo vya kutolea huduma za Afya kuhusu umuhimu wa huduma bora kwa wateja na Waandishi wa Habari.


Timu hiyo pia kwa kushirikiana na Waratibu wa Huduma za Uzazi Mama na Mtoto pamoja Elimu ya Afya kwa Umma ngazi ya Mkoa watashiriki katika kutoa Elimu katika Maoneo ya Masoko ,Nyumba za Ibada ,Vijiwe vya bodaboda nk.


Timu hiyo imewasili katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na kupokelewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa Bw.Ahmed Chibwana.




Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)