Wananchi
wa kijiji cha Mwashigini kata ya Mwakata halmashauri ya Msalala wilayani Kahama
Mkoani Shinyanga wamechangia zaidi ya shilingi milioni tatu kwa ajili ya ujenzi
wa zahanati ya kijiji hicho.
Hayo
yamesemwa na diwani wa kata ya Mwakata Ibrahim Six Masanja wakati akizungumza
na Gimu Blog.
Masanja
amesema kuwa katika mchango huo kila kaya imechanga kwa shilingi elfu 10 huku
mfuko wa jimbo kupitia kwa mbunge wa
jimbo la Msalala Ezekiel Maige
umechangia Zahanati hiyo.
Hata
hivyo Diwani huyo amesema kuwa kazi ya ujenzi wa zahanati unaendelea baada ya
maji ya ujenzi kupatikana katika kipindi hiki cha masika .
Sanjari
na hayo Masanja amesema kuwa kuna zaidi ya bati
2000 na tofali 30 elfu katika kata yake zilizotokana na msaada wa maafa
ya mvua ya barafu Mwakata.