Wananchi wa kata ya Lunguya halmashauri ya Msalala
wilayani Kahama Mkoani Shinyanga wamelalamikia kutokana na kituo cha Afya cha
Lunguya kukosa vifaa muhimu ikiwa ni pamoja na mipira ya kujifungulia kwa akina
mama wajawazito.
Wakizungumza
katika mkutano wa hadhara wananchi hao wamesema kuwa suala la mipira katika
kituo hicho imekuwa changamoto kwao ambapo hununua kwa shilingi elfu 3000 karibu na eneo la kituo hicho.
Aidha
wananchi hao wameomba serikali kuongeza
idadi ya watumishi katika kituo hicho kwani kinahudumia wakazi wengi .
Akijibu
hoja hiyo diwani wa kata ya Lunguya
Benedict Manuary amesema kuwa kutozwa mpira wa kujifungulia kwa akina
mama wanaojifungua linakwendana kinyume na matakwa ya serikali na kuwaomba
wananchi kutoa ushirikiano pindi wanapokumbwa na matatzizo.
Naye
mbunge wa jimbo la Msalala amesema kuwa ni vyema kuyaripua mapema mafisadi
kabla hayajaota mizizi huku akishangazwa kwa kituo hicho kukosa vipimio vya
kupimia magonjwa madogo madogo kama vile malaria .
WANANCHI NI JAMBO LA BUSARA KUPAMBANA NA MIMBA PAMOJA NA UTOAJI WA MIMBA
JibuFuta