KUTOA TAARIFA PEKE YAKE HAKUTOSHI KUBADILI TABIA; MAARIFA, MOTISHA NA MAZINGIRA RAFIKI NI MUHIMU.

MUUNGANO   MEDIA
0



Imebainika kuwa ili jamii iweze kubadili tabia na kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya, haitoshi kutoa taarifa pekee, bali ni muhimu kuelewa vikwazo vinavyowazuia watu kubadili tabia zao.

Akizungumza katika mwendelezo wa mafunzo ya Uelewa wa Tabia (Behavioral Insights) kwa waratibu wa elimu na hamasa ya afya katika afya ya uzazi, mama na mtoto mkoani Kigoma, Jery Bikyeombe kutoka Shirika la Afya Duniani( WHO) Tanzania amesema kuwa swali la msingi katika kubadili tabia ni: "Ni nini kinachokuzuia kubadili tabia.



Ameeleza kuwa mara nyingi vikwazo hivyo hugawanyika katika maeneo makuu matatu ambayo ni ukosefu wa maarifa (Knowledge), ukosefu wa motisha (Motivation), na mazingira au huduma zisizorahisisha kufanya maamuzi sahihi (Convenience).

Kwa mujibu wa Bikyeombe, mtu anaweza kuwa na taarifa sahihi kuhusu huduma za afya lakini akakosa motisha ya kuzitumia, au akashindwa kuzifikia kutokana na umbali wa huduma, muda, gharama au changamoto nyingine za mazingira.

Amesisitiza kuwa matumizi ya mbinu za Uelewa wa Tabia husaidia kubaini sababu halisi zinazowafanya wananchi wasitumie huduma za afya, hatua inayowezesha kubuni afua zinazojibu mahitaji halisi ya jamii badala ya kutegemea utoaji wa elimu pekee.

Aidha, amewahimiza Waratibu wa elimu na hamasa ya afya kutumia mbinu hizo katika kuandaa kampeni na ujumbe unaolenga kuondoa vikwazo vinavyozuia wananchi kutumia huduma mbalimbali za afya, ikiwemo huduma za uzazi wa mpango, afya ya mama na mtoto pamoja na kuhamasisha mtindo bora wa maisha na kuifanya jamii.kuwa.na.Fikra pevu zaidi.

Halikadhalika, amesema mila na desturi  kwenye jamii pia huchangia kuwa kikwazo cha mabadiliko ya tabia.

Mafunzo hayo yanaendelea mkoani Kigoma yakilenga kuimarisha uwezo wa Waratibu wa elimu na hamasa ya afya kutumia mbinu za Uelewa wa Tabia ili kuongeza matumizi ya huduma za afya na kuleta mabadiliko chanya ya tabia katika jamii.



Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)