MFAHAMU KOCHA MZAWA ABUBAKARI ALLY FRANCIS (ABOUJR)

MUUNGANO   MEDIA
0


 Abou Anahudumu katika kikosi cha Fountain gate Fc kama Caretaker Bara baada ya timu kuwa katika hali tete ya kushuka Daraja.


Aboujr anahudumu katika timu za vijana za Fountain gate Academy akifundisha vijana wa U17,,U20 na Program maalumu za vijana msimu wa 2024/2025 katika ligi ya Vijana TFF (NBC YOUTH LEAGUE) amefanikiwa kufika fainal akitoka katika kundi B kundi ambalo lilikuwa na Timu 8 sambamba na Mkongwe Simba.


Na baadae kwenda katika hatua ya 8 bora ambapo kulikuwa na vigogo wote wa Kariakoo Simba na Yanga na Matajiri wa Chamazi Azamfc ambapo pia alifanikiwa kufika fainal ambapo ilikuwa AzamFc vs Fountain gate U20.


Baada ya hapo Rais wa Club Japhet Makau aliamua kumpandisha na kwenda kuisaidia Timu kubwa katika harakati za kuinasua timu kubaki Ligi kuu Tanzania Bara ambapo amesimamia Michezo 4 dhidi ya Tanzania Prison Nyumbani na Ugenini na Dhidi ya Stand united Nyumbani na Ugenini na kufanikiwa kuibakisha Timu Ligi kuu ABOUJR Ana leseni CAF DIPLOMA B.


Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)