Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mhe.Kenani Kihongosi leo Julai 20, 2025 Jijini Dodoma wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mhe.Kihongosi amesema miradi ambayo imekamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi walliokuwa na kiu kubwa ya kupata huduma za kijamii zikiwemi za Afya, Maji, Umeme na Barabara kwenye maaeneo yao.
Amesema Serikali kwa kuzingatia Ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na Mipango ya Maendeleo ya Kitaifa imeweza kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora, kwa gharama nafuu na kwa wakati.
“Katika Awamu ya Sita Mkoa wa Arusha umepokea na kukusanya fedha kiasi cha shilingi Trilioni 3.5, ambazo zimetumika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo kwenye sekta mbalimbali,” amesema Kihongosi.
Amesema mafanikio mengine ni katika sekta ya Afya ambapo Serikali imetoa jumla ya shilingi Bilioni 94.2 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwa kujenga na kuboresha miundombinu ya afya, ununuzi wa dawa na vifaa tiba.
.jpg)

