SEKTA YA MADINI YAFANIKIWA KUVUKA LENGO LA KUCHANGIA ASILIMIA 10.

MUUNGANO   MEDIA
0

 




Na Avelina Musa - Dodoma.


Sekta ya Madini imefanikiwa kuvuka lengo la kuchangia asilimia 10 kwenye Pato la Taifa mwaka mmoja kabla ya muda ulioainishwa katika Sera ya Madini ya Mwaka 2009 na kwenye Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2021/2022 hadi 2025/2026.

Hayo yameelezwa Leo Mei 02.2025 na Waziri wa Madini Mhe,Anthony Mavunde wakati akiwasilisha Makadirio ya bajeti ya wizara kwa mwaka wa fedha 2025/2026  Bungeni Jijini Dodoma


Mhe, Mavunde amesema  mapato ya fedha za kigeni kupitia Sekta ya Madini, ukusanyaji wa mapato hayo umekuwa ukiimarika mwaka hadi mwaka ambapo Mwaka 2024 thamani ya mauzo ya madini nje ilikuwa dola za Marekani milioni 4,119.9 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 3,551.4 mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 16.0.

 "Hii ilichangiwa na kuongezeka kwa mauzo ya dhahabu ambapo thamani ya mauzo ya dhahabu iliongezeka kwa asilimia 11.8 na kufikia dola za Marekani milioni 3,419.6 mwaka 2024 ikilinganishwa na dola za Marekani milioni 3,058.9 mwaka 2023"Amesema Mhe Mavunde.

Aidha, mauzo ya madini yalichangia asilimia 60.0 ya mauzo yote ya bidhaa zisizo asilia.Mheshimiwa Spika, katika Mwaka 2024, jumla ya vibali 9,540 vya kuuza madini nje ya nchi vilitolewa ikilinganishwa na vibali 8,809 vilivyotolewa Mwaka 2023. 

Ongezeko la vibali hivyo kwa kiasi kikubwa limetokana na kuongezeka kwa uhitaji wa madini ya vito, makaa ya mawe, dhahabu na kinywe nje ya nchi. Aidha, katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, jumla ya vibali 116 vyenye thamani ya dola za Marekani 14,813,664.38 vya uingizaji madini nchini vilitolewa ikiwa ni hatua mojawapo ya kusimamia na kudhibiti biashara ya madini nchini.

Mhe,Mavunde amesema katika kuendeleza Madini Muhimu na Madini Mkakati  jitihada mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na Serikali ili kuhakikisha madini muhimu na mkakati yananufaisha Taifa ambapo  Jitihada hizo ni pamoja na kufanya tafiti, kuhamasisha uwekezaji, kutoa leseni za utafutaji, uchimbaji, uchakataji, uongezaji thamani na biashara ya madini ya kimkakati na madini muhimu na kutangaza fursa za uwepo wa madini nchini kupitia Mining Vision 2030: Madini ni Maisha na Utajiri. 

Mwisho.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)