KATIKA KIPINDI CHA JULAI 2024 HADI MARCH 2025 WACHIMBAJI WADOGO 127 WAPATA MIKOPO.

MUUNGANO   MEDIA
0

 





Na Avelina Musa - Dodoma.

Wizara ya Madini  kupitia taasisi zake imeendelea kuwahamasisha wachimbaji wadogo kuanzisha vikundi katika shughuli za madini na kutunza kumbukumbu za uzalishaji na biashara za madini ikiwa ni miongoni mwa vigezo vya kuwawezesha kupata mikopo kwenye taasisi za fedha.

 Katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025 jumla ya shilingi 51,422,401,572.00 zilikopeshwa kwa wachimbaji wadogo 127. 


Hayo yameelezwa Leo Mei 02.2025 na Waziri wa Madini Mhe,Anthony Mavunde wakati akiwasilisha Makadirio ya bajeti ya wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2025/2026  Bungeni Jijini Dodoma.


Mhe,Mavunde amesema Wizara ya Madini kupitia (STAMICO) imeendelea kuratibu shughuli za uchimbaji mdogo kwa kutoa huduma za kitaalamu kwa wachimbaji wadogo katika nyanja za utafiti, uchimbaji, uchenjuaji madini pamoja na utunzaji wa mazingira. 


Amesema katika kipindi cha Julai 2024 hadi Machi 2025, jumla ya wachimbaji wadogo 471 wamepatiwa mafunzo kupitia vituo vya mfano vya Katente, Lwamgasa na Itumbi ambapo mpaka sasa wachimbaji 12 wa madini wameanzisha vituo vyao baada ya kujifunza kupitia vituo hivyo. 


Aidha, kupitia vituo vya mfano, huduma ya uchenjuaji mbale za dhahabu kwa wateja 41 ilitolewa ambapo dhahabu ya uzito wa kilogramu 119.57 yenye thamani ya shilingi 23,318,849,170.45 ilichenjuliwa.


"Katika kuwasaidia wachimbaji wadogo kupata taarifa za jiolojia, huduma za uchorongaji kwa gharama nafuu zilitolewa kwa wachimbaji wadogo 14 katika maeneo ya Tambi–Mpwapwa, Nyawa–Bariadi, Matondo, Makongolosi na Matundasi–Chunya, Lwamgasa, Nyaruyeye, Nyakagwe na Nyamalimbe–Geita, Endabash-Karatu pamoja na Mavota–Biharamulo. Jumla ya mita 3,306.47 zimechorongwa katika maeneo hayo.Amesema Mhe,Mavunde.

Mwisho.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)