WAATHIRIKA WA MAAFA HANANG MKOANI MANYARA WASHIKWA MKONO NA WAANDISHI WA MICHEZO TANZANIA

MUUNGANO   MEDIA
0

Wakati huu ambao Taifa la Tanzania likiwa linazizima kwa vilio na majonzi kwa kushuhudia Watanzania wenzetu wa mkoa wa Manyara wakisongwa na zimwi jeusi la mafuriko yaliyoacha maafa makubwa.


- Wakati huu Tanzania ikiazimisha miaka 62 ya Uhuru wake huku katikati ya mioyo ya watu wake wakiwa na maumivu makali ya kushuhudia ndugu,jamaa,rafiki wa Manyara wakiangamia kwa mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizoandamana na mafuriko ya matope.


Hakika bendera zinapepea kinyonge nusu mlingoti.


- Pamoja na maumivu bado Watanzania wa kada mbali mbali wakiongozwa na Rais wa Jamuhuri Ya Muungano wa Tanzania Daktari Samia Suluhu Hassan wameendelea kuikimbilia Manyara na Wana Kateshi na Hanang kuwashika mkono na kuwapa  pole na kuendelea kuwafuta machozi.


Umoja wa Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania wakiongozwa na baadhi ya Waandishi 'waandamizi' Twalib Muwa, Charles Abel, Devotha, Abdul Mkeyenge, Akida Akida, Juma Ayo na wengine wameweza kujitokeza na kufikisha msaada wa pole kwa wana Manyara kupitia kwa Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo, Ndugu Damas Dumbaro ili iweze kuwafikia walengwa.


Upande wa pili wadau walioshurikiana na Waandishi wa Michezo kwa ukaribu ni kampuni ya Water Com pamoja na kampuni ya ulinzi ya Bullet Security pamoja na wadau wengine.


Na kwa upande wa Waziri Damas Dumbaro kwake kwa niaba ya Serikali amewashukuru Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania kwa namna walivyoguswa na kujitolea kidogo walichonacho kwa ajili ya kusimama pamoja na wana Manyara.


Na shughuli hii ya kukabidhi msaada imefanyika Jijini Dar es Salaam ulipo uwanja wa Benjamin Mkapa huku ukishuhudiwa na viongozi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) pamoja na Mwenyekiti wa bodi ya ligi Steven Mguto.


Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)