HCD MTAA KWA MTAA

MUUNGANO   MEDIA
0






































Tarehe 30, Aprili,2025 timu ya Mafunzo ya HCD yanayolenga kushirikisha jamii kwa kutumia mbinu Bunifu na Shirikishi katika kutatua changamoto zinazopelekea jamii kuwa na mtazamo hasi kuhusu umuhimu wa huduma za chanjo imetembelea katika mitaa mbalimbali kata ya Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga na kufanya majadiliano na makundi mbalimbali ili kuongeza ufanisi huduma za chanjo.


 Baadhi ya makundi muhimu yaliyofikiwa na kutoa maoni ni pamoja na viongozi wa dini, viongozi wa Jeshi la Jadi(Sungusungu),viongozi wa vitongoji na vijiji, wafanyabiashara, wakulima.


Hata hivyo, kupitia majadiliano hayo makundi hayo yameweza kutoa maoni tofauti kuhusu huduma za chanjo.


Lengo la majadiliano hayo ni kupata maoni na kuweka mikakati ya pamoja ili jamii iwe na mwitikio kuhusu umuhimu wa huduma za chanjo.

 


Ikumbukwe kuwa Mafunzo ya HCD ni mfumo bunifu inayoshirikisha jamii moja kwa moja hadi hatua za mwisho kutatua changamoto katika jamii ili kuwa na uelewa wa pamoja kwenye utatuzi wa changamoto hiyo.



                                        MWISHO.
 

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)