WATANZANIA WATAKIWA KUMNADI NA KUMWOMBEA PROF.MOHAMED JANABI ILI ASHINDE KATIKA UCHAGUZI WA MKURUGENZI WHO KANDA YA AFRIKA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 




Na Avelina Musa - Dodoma.

Serikali kupitia Wizara ya Afya  imewataka watanzania kumnadi na kumuombea Mgombea wa nafasi ya Ukurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika 

Proffesa Mohamed Janabi ili ashinde nafasi hiyo.

Kauli hiyo imetolewa leo Machi 22,2025 jijini Dodoma na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama wakati akimtambulisha Mgombea wa nafasi ya Ukurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika Profesa Mohamed Janabi

"Kampeni za wagombea wa nafasi hii tayari zimeshaanza kwa njia mbalimbali, nasi hatuna budi kushirikiana kumnadi mgombea wetu kwa nguvu, ari na morari kubwa. Nitoe rai kwa wananchi, mashirika na wadau wa Sekta wa ndani na nje kuungana pamoja katika kumnadi na kumuombea dua mgombea wetu, " amesisitiza Mhagama


Mhe,Mhagama amesema Taifa letu lina sifa ya kutoa viongozi wenye weledi katika nyanja mbalimbali, na tunajivunia kwamba Prof. Janabi yuko tayari kulihudumia Bara letu katika nafasi hii kwa ustadi wa hali ya juu.

Waziri Mhagama amesema kutokana na kukua kwa kasi kwa mahusiano mazuri ya Kidiplomasia pamoja na ushirikiano ambao Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuimirisha baina ya nchi ya Tanzania na Mataifa mengine, jambo hilo linaipaisha Tanzania kwenye majukwaa ya Kikanda na Kimataifa.

 "uzoefu wa Prof. Janabi katika masuala ya ugharamiaji wa huduma za afya kwa kuzingatia kipindi hiki ambacho Dunia inapita katika changamoto ya kubuni vyanzo vya uhakika katika ugharamiaji wa huduma za afya na uzalishaji wa bidhaa za afya nchini pamoja na usimamiaji wa mifumo ya utoaji wa huduma za afya zinatupa nafasi kubwa ya kushinda nafasi hii, "amesema Mhagama

Aidha, Mhagama amesena uzoefu wake umedhihirika katika kuzuia, kudhibiti na kupambana na magonjwa ya mlipuko pamoja na magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa yakiongezeka kwa kasi kubwa ulimwenguni.

Waziri Mhagama amesema serikali ina imani kubwa juu ya Prof. Janabi
Katika nafasi hiyo kwani ameshafanya Mapinduzi makubwa katika sekta ya Afya ndani ya nchi na nje ya nchi.

"Tuna imani kuwa kwa uongozi wake, Afrika itapiga hatua kubwa katika kuboresha mifumo ya afya, kupambana na magonjwa, na kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma bora za afya," amesema Mhagama

Hata hivyo,Mkurugenzi wa Kanda anachaguliwa kwa kura ya siri katika kikao cha ndani cha Kamati ya Kanda ya WHO kwa Afrika, ambayo ilikutana Januari 14, 2025, na kuamua kutumia utaratibu wa haraka, kumpata Mkurugenzi wa Kanda badala ya mchakato wa kawaida ambayo huchukua muda mrefu na uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika Mei 18, 2025.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)