SERIKALI YAFANYA MAGEUZI MAKUBWA KATIKA SEKTA YA USAFIRISHAJI KWA KUKIWEZESHA NIT KUTOA MAFUNZO YA URUBANI.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


            Na Avelina Musa - Dodoma.

SERIKALI imefanya mageuzi makubwa katika sekta ya usafirishaji kwa kukiwezesha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) kukamilisha maandalizi ya utoaji wa mafunzo ya Urubani Nchini.

 Ambapo Chuo kimekamilisha matakwa ya kupata ithibati kutoka TCAA na hivyo mafunzo hayo yanatarajiwa kuanza mwezi Mei 2025.

Hayo yamesemwa Leo march 20.2025 na Mkuu wa Chuo cha NIT Dkt.Prosper Mgaya,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa chuo hicho katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

"Katika kukiwezesha Chuo hicho kuanza mafunzo hayo Serikali mpaka sasa imetoa jumla ya takribani bil.6."Amesema Dkt.Prosper.

Dkt.Prosper amesema kuanzishwa kwa mafunzo haya hapa nchini kutapunguza gharama ya mafunzo kwa takribani asilimia 50 – 60 ambazo watanzania wengi wanatumia kupata mafunzo hayo nje ya nchi.

Aidha amesema mafunzo hayo yataongeza idadi ya marubani wazawa hivyo kutapunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi kwa marubani wa kigeni ambao gharama yake ni kubwa.

"Ifahamike kuwa kama nchi tumekuwa tukitegemea kwa kiasi kikubwa kupelekea watanzania kupata mafunzo ya urubani nje ya nchi hivyo Serikali na watanzania kwa ujumla tumekuwa tukitumia fedha nyingi sana za kigeni kusomesha marubani nje ya nchi"Amesema Dkt. Prosper.

Ameeleza kuwa mafunzo ya urubani yanahitaji kuwa na wakufunzi na vifaa vya kufundishia vinavyokidhi vigezo vya kimataifa. 

“Katika kuhakikisha Chuo kinaanza mafunzo ya Urubani Serikali imegharamia mafunzo ya wakufunzi watano ambao wamepata mafunzo haya nchini Afrika ya Kusini kwa Gharama ya bil. 1.5 ikiwa ni wastani wa T Mil.300 kwa kila mkufunzi.

Hata hivyo amesema Serikali imenunua ndege mbili za mafunzo aina ya Cesna 172 zenye injini moja ambazo tayari zipo nchini kwaajili ya kuanza mafunzo hayo.

“Ndege hizi zina thamani ya sh.bil 2.9 na serikali ipo katika taratibu za ununuzi wa ndege nyingine tatu ikiwa ndege moja ya injini mbili ambayo itawasili mwezi Oktoba 2025 ambayo ina thamani ya bil.5.9, na Ndege mbili za injini moja zitawasili mwaka 2026.Amesema Dkt.Prosper.

Mwisho.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)