Na Avelina Musa - Dodoma.
Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA)imesema katika kipindi cha miaka minne ya serikali ya awamu sita imefanikiwa kutoa jumla ya vyeti 7,679 vya uthibitisho wa umiliki wa hakimiliki kwa wabunifu waliosajili kazi zao.
Hayo yameelezwa na Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania (COSOTA) Bi.Doreen Anthony Sinare wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Taasisi hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita Leo Machi 21, 2025, jijini Dodoma.
Bi.Doreen amesema wasanii na waandishi watanufaika na jumla ya kiasi cha Tsh. 593,589,915.98 zilizokusanywa kwa kipindi cha mwaka 2023/2024.
"Gawio la Serikali ni 142,810,524.14 na gharama ya uendeshaji COSOTA ni 285,621,048.29,muundo wa COSOTA kwa sasa unaruhusu uanzishwaji wa Makampuni ya Wasanii ya kukusanya na kugawa mirabaha (Collective Management Organization - CMO) na COSOTA kubaki kama msimamizi wa masuala ya hakimiliki na kusimamia Kampuni hizo,"ameeleza.
Bi.Doreen amesema marekebisho ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 2022 yalipelekea kuandaliwa kwa Kanuni ya Kuanzishwa kwa Makampuni ya kukusanya na kugawa Mirabaha na kuruhusu uanzishwaji wa Makampuni kwa ajili ya kusimamia haki mbalimbali za aina za kazi za Sanaa na Uandishi .
"Kwa mwaka 2021 - 2025 COSOTA imefanikiwa kufanya migao miwili kama alivyoahidi Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alipolihutubia bunge mwaka 2021 ambapo alisisitiza katika kipindi cha uongozi wake, serikali itahakikisha wabunifu wote wananufaika zaidi na kazi zao, "amesema
Aidha, akifafanua kuhusu mgao huo amesema Mgao wa kwanza ambao ulikuwa ni mgao wa ishirini na tatu ulifanyika tarehe 28/01/2022 na ulikuwa wa kiasi cha Tshs. 312,290,259,000, ambapo Wasanii 1,123 walinufaika, na ulitokana na matumizi ya kazi 5,924 za muziki ambazo zilitumika katika vituo 11 vya redio, ikiwemo redio katika ngazi ya kitaifa, Mkoa, wilaya, kijamii na za kidini.
Bi.Doreen amesema marekebisho ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki ya mwaka 2022 yalipelekea kuandaliwa kwa Kanuni ya Kuanzishwa kwa Makampuni ya kukusanya na kugawa Mirabaha na kuruhusu uanzishwaji wa Makampuni kwa ajili ya kusimamia haki mbalimbali za aina za kazi za Sanaa na Uandishi .
"Kwa mwaka 2021 - 2025 COSOTA imefanikiwa kufanya migao miwili kama alivyoahidi Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan alipolihutubia bunge mwaka 2021 ambapo alisisitiza katika kipindi cha uongozi wake, serikali itahakikisha wabunifu wote wananufaika zaidi na kazi zao, "amesema Bi Doreen.
Mwisho.