RAIS SAMIA ATOA MAAGIZO MAMLAKA YA SERIKALI ZA MITAA.

MUUNGANO   MEDIA
0



Na Mwandishi wetu - Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa serikali za mitaa nchini kujiepusha kuwa vyanzo vya migogoro ya ardhi kwenye maeneo yao, akiwataka kuwa sehemu ya masuluhisho ya migogoro hiyo.



Mhe.Rais ameyasema hayo wakati akizungumza katika mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT),uliofanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete.


"Watu wote wanakimbia kwenda kuchukua fomu na mnatuacha Serikali za mitaa hazina Viongozi,hazina wasimamizi na kujaza watu ambao hawana experience (uzoefu) lakini tukijua mapema tutawaandaa viongozi mapema kwa kuwapa miongozo na kuwafanyia mafunzo ili wawe tayari kukabiliana na uchaguzi,sasa usiposema mapema ukajakuchukua fomu mbele umekosa yote,umekosa nafasi na cheo utakiacha." Alisema.


Aidha,Mhe. Dkt. Samia amewapa onyo kali Wakurugenzi,Wakuu wa Wilaya na Viongozi wote waliochini ya Mwamvuli wa Serikali za mitaa kwa kuwataka kutoa taarifa mapema kwa wanaotaka kurudi kwa wananchi na kuomba ridhaa ya kuwaongoza ili viongozi walio chini yao wapandishwe hadhi na kushikilia nafasi zao badala ya kuacha Serikali za mitaa bila viongozi na kuongeza kuwa kwa atakaye fanya hivyo bila kutoa taarifa basi ajiandae kukosa yote kwa kupoteza cheo na kuiacha nafasi aliyokuwa akiitumikia.


Hata hivyo amewatakia kheri wote wanaotaka kutangaza nia na kusema wote watakao fata utaratibu wa kutoa taarifa za awali na wakakosa nafasi walizogombea Serikali itawafikiria.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) Bw.Murshid Hashim Ngeze amesema kuwa ALAT imetekeleza vizuri usimamizi wa pesa za maendeleo kupitia pesa za miradi ya maendeleo zilizopelekwa kwenye Serikali za Mitaa kwa ushirikiano mkubwa na Wakuu wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi na Madiwani kiasi kwamba hoja za ukaguzi zinapungua kila mwaka na kuongeza kuwa kupitia maagizo ya Rais wameimarika kwa kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria ,Kanuni na miongizo ya ALAT kiasi kwamba wameenda mbali zaidi na kuhuisha Sheria ya uanzishaji wa ALAT kupitia Mkutano huo.


Mwisho.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)