TRA YAPATA MAFANIKIO LUKUKI KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na Avelina Musa - Dodoma.


MAMLAKA ya Mapato Tanzania ( TRA), imefanya kazi kubwa ya kupambana na wafanyabiashara haramu wanaokwepa kodi kupitia bandari bubu katika miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.


Hayo yameelezwa Leo march 12.2024 na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuh Mwenda Jijini Dodoma juu ya mafanikio ya Mamaka hiyo kwa kiindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.


Amesema kutokana na kuwepo kwa bandari bubu wapo baadhi ya wafanya biashara ambao huingiza bidhaa kimagendo, wakati mwingine kuchepusha bidhaa badala ya kuvusha nje ya nchi kama vibali vinavyowataka na kurudisha bidhaa ndani.


Amesema TRA imejiimarisha zaidi katika kupambana na uhalifu huo na wale wanaobainika wanachukuliwa hatua kali za kisheria pamoja na kulipishwa faini.


Pia amesema ndani ya miaka minne Mamlaka hiyo imeweza kukusanya mapato kiasi cha Sh. Trilioni 21.2 sawa na asilimia 78.

Amesema kwa kipindi kama hicho kabla ya uongozi wa Rais Samia TRA ilikuwa na makusanyo ya Sh. Trilioni 11.12.


Amesema kuongezeka kwa mapato hayo ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuhimarisha mahusiano mema na wafanya biashara kwa kuboresha huduma kwa wafanyabiashara hao.


Mafanikio ndani ya miaka minne yaliyotokana na utekelezaji wa Maagizo ya Mhe. Rais Dkt. Samia, Suluhu Hassan:Kusimamia uadilifu kwa Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na kuchukua hatua kwa mujibu wa Sheria kwa wachache wanaokiuka maadili ya utumishi wa umma pamoja na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa watumishi wote wa TRA unaotokana na weledi na uwajibikaji uliosisitizwa na Mheshimiwa Rais.


"TRA katika kipindi cha miaka minne, imechukua hatua zifuatazo kwa wachache wanaoenda kinyume na maadili 1. Kufukuzwa kazi -14,2. Kushushwa Mshahara- 6,3. Kushushwa cheo na kupunguzwa mshahara- 12,4. Kupewa Onyo la Maandishi - 22",amesema.


Mwisho.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)