Wizara ya afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na wadau wanafanya kikao kazi cha kuandaa Mwongozo wa uchunguzi wa awali wa afya na lishe kwa wanafunzi shuleni.
Kikao kazi kinafanyika mkoani Dodoma na kimeanza tangu tarehe 12 hadi 16,Agosti, 2024.
Lengo la Mwongozo huu ni kubaini changamoto mbalimbali za kiafya na lishe kwa wanafunzi na kuzitatua kwa kumpa rufaa mwanafunzi kwenda katka kituo cha kutolea huduma za afya kilichopo karibu na shule ili kupata huduma stahiki.
Ikumbukwe kuwa
Lishe bora huimarisha Afya ya Uzazi kwa vijana wa rika balehe ambapo wanafunzi ni mojawapo ya kundi hili muhimu.
Aidha, lishe duni kwa vijana wa rika balehe inatajwa kuwa chanzo cha matatizo ya afya ya uzazi miongoni mwa wanawake na wanaume.
Upungufu wa virutubisho muhimu kwa watoto na vijana unaelezwa kuathiri via vya uzazi.
Udumavu, uzito pungufu, ukondefu, uzito kupita kiasi na unene ni changamoto zinazowakabili watoto na vijana wenye umri wa miaka mitano hadi kumi na tisa nchini hivyo, Serikali imeendelea kuwekeza nguvu suala la elimu ya lishe katika maeneo mbalimbali ikiwemo shuleni kwani lishe duni husababisha pia vijana kutofanya vizuri darasani.
#UsibakiNyuma #MtuNiAfya
Fanya kweli Usibaki nyuma,Mtu ni Afya.
Kwa taarifa,Elimu na Ushauri zaidi Piga Simu 199
@ummymwalimu
@mohamed_mchengerwa
@dr_mollel
@ntulikapologwe
@onamachangu
@wizara_afyatz #afyanimtaji
@azamtvtz
@ortamisemi
@latra_tz
@polisi.tanzania
@unesconatcomtz
#elimuyaafyakwaumma