Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Norman Jonas ametoa wito kwa watumishi wa Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kushirikiana, kufanya kazi kwa bidii na ubunifu ili kuweza kufikisha Elimu ya Afya kwa Jamii.
Ameyasema hayo leo Agosti 14, 2024 katika kikao cha makabidhiano ya ofisi na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Ona Machangu.
"Kinga ni muhimu katika Afya na elimu inaanza kwanza. Ili mtu achukue hatua za kujikinga dhidi ya Magonjwa mbalimbali na kwa mantiki hiyo suala la elimu ya afya ni suala muhimu sana hivyo sisi watumishi wa afya ni vyema kufanya kazi kwa ushirikiano, bidii na ubunifu zaidi ili kuleta matokeo chanya"amesema.
Kwa upande wake aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Dkt. Ona Machangu amewashukuru watumishi wote kwa kumpatia ushirikiano katika kipindi cha uongozi wake na kuwaomba waendelee kwa kumpatia ushirikiano kiongozi mpya.
Kwa upande wao Wajumbe wa kikao hicho wamepongeza Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kwa kupewa nafasi ya kuongoza sehemu hiyo na kumuahidi kutoa ushirikiano.
MWISHO.