KIKAO CHA KUANDAA NA KUPITIA VIELELEZO VYA KUELIMISHA JAMII KUHUSU KUJIKINGA NA UGONJWA WA TRAKOMA NA USUBI CHAENDELEA MKOANI MOROGORO.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Leo Agosti 14, 2024 Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa hayapewi Kipaumbele chini ya Wizara ya Wizara ya Afya ikishirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI wameendelea na Kikao cha kuandaa vielelezo vya kuelimisha Jamii kuhusu Kujikinga na Ugonjwa wa Trakoma na Usubi ikiwa leo ni Siku ya tatu.


Katika Kikao hicho ,Wizara ya Afya, kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa Yaliyokuwa Hayapewi Kipaumbele pamoja Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa Kushirikiana na Wadau wa Save the Children -Act to END NTDs East inaandaa vielelezo vya kuelimisha jamii ili iweze kujikinga na Magonjwa hayo kwa kushiriki kwenye afua za kumeza Kingatiba kila zinapotolewa kwenye jamii .


Afua zingine ni kuwa na desturi ya kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni, kujenga choo bora na kukitumia, usafi binafsi na usafi wa mazingira.


Leo Wataalamu wa Maudhui na Wasanifu wa Picha wanajadili kuhusu vielelezo vya Mitandao ya Kijamii ambapo Mkuu wa Programu ya Mawasiliano ya Afya na Mabadiliko ya Tabia katika Jamii kutoka Wizara ya Afya, Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma Peter Mabwe amezungumzia umuhimu wa kuwa na Maudhui yenye jumbe fupi fupi kwenye mitandao ya Kijamii.


"Wasomaji mitandaoni huwa hawahitaji mambo mengi ,wanataka ujumbe mfupi, unaovutia na kueleweka, hivyo ni muhimu kuzingatia hilo"amesisitiza.


Ikumbukwe kuwa kikao hicho kinafanyika kwa siku 5 kuanzia tarehe 12 hadi 16, Agosti, 2024.


MWISHO.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)