WAZIRI JAFO ATOA MAELEKEZO USAFI WA FUKWE

MUUNGANO   MEDIA
0


 Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.

Selemani Jafo amewahimzia wawekezaji wanaowekeza katika fukwe

mbalimbali nchini kuhakikisha zinakuwa safi ili kutunza mazingira.

Dkt. Jafo ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Asubuhi

Hii kinachorushwa na kituo cha Radio cha TBC Taifa leo tarehe 19 Machi,

2024.

Amesema kuwa kumekuwepo na changamoto ya uchafu katika fukwe nyingi

nchini hususan chupa za plastiki zilizotumika ambazo si tu husababisha uchafu

wa mazingira lakini pia ni kero kwa wageni wanaozitembelea.

Kutokana na hali amezielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa ambako fukwe

hizo zinapatikana, licha ya shughuli mbalimbali za utunzaji wa mazingira

wanazotekeleza pia zisimamie shughuli za usafi wa mazingira katika maeneo

hayo.

Waziri Dkt. Jafo ameongeza kuwa halmashauri hizo ziwe na mpango wa

kushirikiana na vijana wanaojitolea kuikota chupa zinazotupwa katika fukwe

kwa kuwapa motisha hivyo maeneo hayo kuendelea kuwa safi.

Pamoja na kutoa pongezi kwa viwanda vinavyorejeleza chupa za plastiki

amewahimiza wenye viwanda wengine kuchukua hatua hiyo ambayo itasaidia

katika kuondosha taka za chupa katika fukwe.

Amesema Ofisi ya Makamu wa Rais inashirikiana bega kwa bega na wadau

mbalimbali kuwahamasisha kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha mazingira

kwenye fukwe nchini zinakuwa safi.

Kwa upande mwingine Waziri Dkt. Jafo amewataka wenye magari kuwa na

vyombo maalumu vya kuhifadhia taka badala ya kutupa ovyo njiani ili kutunza

mazingira ya barabarani.

“Tuna kazi kubwa ya kutengeneza ustaarabu, utakuta mtu akiwa kweny basi

anakunywa maji anatupa chupa nje na inazagaa ovyo na kuchafya mazingira

hivyo tunawataka wenye magari na wenye mabasi wote kuwa ‘dustbin‘ kwa

ajili ya kuwekea taka na wenye magari simamieni zoezi hilo,“ amesisitiza Dkt.

Jafo.

Ikumbukwe kuwa awali kulikuwepo na changamoto ya chupa za plastiki

ambazo hutupwa ovyo na sasa hivi zimekuwa ni malighafi kwa viwanda kwa

ajili ya kurejelezwa.


Kutokana na hatua hiyo Serikali imekuwa ikihamasisha viwanda kufanya

urejelezaji wa chupa za plastiki ambazo huokotwa na kukusanywa katika

maeneo mbalimbali yakiwemo fukwe.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)