Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko, leo amewasili mkoani Mbeya
kwa ziara ya kikazi mkoani humo.
Ziara hiyo pia itahusisha ukaguzi wa miradi mbalimbali ya umeme mkoani humo.
Akiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe, Dkt. Biteko amepokelewa na
viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera.
Katika kikao chake na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Dkt. Biteko ameeleza jitihada zinazofanywa
na Serikali katika nyanja mbalimbali ikiwemo Elimu, Siasa na Nishati.
Katika Sekta ya Nishati, Dkt. Biteko ameeleza kuwa, upungufu wa umeme nchini ni kati ya
megawati 300 hadi 190 lakini kwa sasa kuna matumaini makubwa kwani mradi wa Julius
Nyerere ( JNHPP) unatarajiwa kuingiza megawati 235 katika gridi ya Taifa mwezi huu na
matumaini mengine ni kutoka Mradi wa umeme wa Rusumo ambao utaingiza katika gridi
megawati 27.
Amesema kuwa, kiasi hicho cha umeme kitakapoingia kwenye gridi ya Taifa kitaondoa hali ya
sasa ya mahitaji ya umeme kuwa makubwa kuliko uzalishaji na pia kuiwezesha Serikali
kuendelea kufanya maboresho kwenye miundombinu ya umeme.
Amesema kuwa, kwa Mkoa wa Mbeya ambao mahitaji yake ni kati ya megawati 70 na 74
ambapo kwa sasa wanapata umeme wa megawati 51 na kueleza kuwa, jitihada zinazoendelea
sasa zitapelekea Mkoa huo pia kupata umeme kulingana na mahitaji.
Katika hatua nyingine, Dkt. Biteko amepongeza Mkoa wa Mbeya kwa kufanya vizuri katika
ukusanyaji wa mapato, utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na usimamizi mzuri wa
sekta Elimu ambao watoto wanaostahili kwenda shule wameripoti kwa zaidi ya asilimia 70.
Vilevile, Dkt. Biteko amesisitiza viongozi kufuata agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuwa, tofauti ya itikadi ya vyama vya siasa isifanye
wananchi kuwa maadui bali watu wabishane kwa hoja huku kipaumbele kikiwa ni maendeleo ya
nchi.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, amemueleza Dkt. Doto Biteko
kuwa, shughuli za kiuchumi katika Mkoa huo zinaendelea vizuri na katika mwaka 2023/2024
walifanikiwa kukusanya mapato ya shilingi Bilioni 49 ikiwa ni zaidi ya asilimia 105.
Ameongeza kuwa, utekelezaji wa miradi ya umeme inaendelea vizuri ikiwemo ya upelekaji
umeme vijijini, vitongojini na migodini.
Katika elimu amesema kuwa, Mkoa huo umekuwa na ufaulu mzuri huku watoto wanaopaswa
kwenda shule, wakiripoti kwa zaidi ya asilimia 70.
Caps
moja
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akisalimiana na Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya Juma Homera mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Songwe Februari 19, 2024.
Mbili
Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, akisalimiana na viongozi
mbalimbali wa mkoa wa Mbeya, mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi mkoani humo.
.jpg)
