VIJIJI NANE NGORONGORO KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI MAGERI

MUUNGANO   MEDIA
0

 

SERIKALI kupitia  Wizara ya Maji imesema  imekuwa ikitenga fedha za utekelezaji wa Mradi wa Maji Mageri utakaohudumia Vijiji nane vya Tinaga, Oloirien, Ngarwa, Yasi, Mdito, Mageri, Mugongo na Magaiduru Wilayani Ngorongoro  Mkoani Arusha ambapo hadi sasa jumla ya Shilingi 2,264,520,000.00 zimetolewa.


 Hayo yamesemwa leo Februari 5 2024  bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi  wakati akijibu swali la  mbunge wa Ngorongoro  Emmanuel Shangai ambae aliuliza ni  lini Serikali itatenga fedha za kutosha kwa ajili ya kumaliza Mradi wa Maji Mageri utakaohudumia Vijiji nane Wilayani Ngorongoro. 


Mhandisi Mahundi  amesema Fedha hizo zimesaidia kukamilisha utekelezaji wa banio la chanzo cha maji Orkanjor, ulazaji wa bomba kuu kutoka kwenye chanzo hadi kwenye tenki umbali wa Kilometa 3 na ununuzi wa pampu 2 zenye uwezo wa kusukuma maji lita 2,054,400 kwa Siku.


"Mheshimiwa Naibu  Spika, kazi zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na ujenzi wa matenki Tisa (9) yenye jumla ya ujazo wa lita 2,000,000, uchimbaji wa mitaro na ulazaji wa mabomba ya usambazaji umbali wa Kilometa 80. Aidha, utekelezaji wa mradi huo umefikia wastani wa asilimia 40 na unatarajiwa kukamilika Mwezi Desemba, 2024"amesema Mahundi.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)