Na. Gideon Gregory, Dodoma.Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amewaagiza wasimamizi bonde la mto Wami/Ruvu kuweza kuwabaini watu walioweka makazi ya kudumu ndani ya hifadhi ya mto huo pamoja na kuandaa barua ambayo itaonesha ni kwa muda gani wanatakiwa kuwa wameondoka ndani ya eneo hilo.
DC Shekimweri ametoa maagizo hayo leo Jijini Dodoma wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa barabara na uwekaji wa alama za mipaka (bikoni) katika hifadhi ya bonde la mto huo na kuwataka wabainishe ni idadi ya watu wangapi waliopo na ambao hawatokuwa wameondoka hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
"Yanapokuja masuala ya umma kwenye uhifadhi wa bonde hili hatutokuwa na mzaha na mtu yeyote, kwahiyo atakayepewa barua akapewa muda wa kuondoka azingatie huo muda wa barua, nafanya hivi kwa maelekezo ya Mhe. Rais ya kwamba tusiwabughudhi watu wetu tulizembea wenyewe tukaacha wakaingia wamekaa tayari wanamakazi na jambo hili ni la kisera watu kuwa na makazi lakini kama wapo sehemu sahihi hatupaswi kuwabughudhi na kuwakwaza,"amesema DC Shekimweri
Amesema wanapaswa kujiridhisha na aina ya watu wanao waweka kama walinzi kama kwani wananchi wanao vamia hifadhi hiyo huenda wanakula nao njama za kuingia na kuanza kufanya shughuli zao ikiwemo uchamaji wa mkaa pamoja na ukataji wa miti kama sio watu wa kuajiliwa kwa masharti ya kudumu waone umuhimu wa kuajili wafanyakazi wa ajira za muda na kuwabadirisha.
"Ni muhimu pia kuangalia namna ya kuwa na ulinzi shirikishi wa hii hifadhi jamii ya watu wanao zunguka hii hifadhi baadala ya kuwa watu wanao vamia maeneo wanaweza kuwa watu wanao linda kwahiyo fikilieni program za kuanza kuwashirikisha kwamfano mnaweza kuwa na mabwawa mkaanzisha kikundi cha vijana wakawa wanaingia humu wanafuga samaki wakapata kipato ili wawe wanahusika katika kutoa taarifa zozote za uvumizi wowote wa bonde,"amesema DC Shekimeri.
Kwa upande wake Mwakilishi wa mkurugenzi wa rasilimali za maji Wizara ya Maji Joseph Mrimoto amesema kila mmoja anapaswa kulinda hifadhi hiyo kwani ndiyo mboni ya mkoa wa Dodoma na kutoa rai kwa vijiji vyote vinavyozunguka eneo hilo kuhakikisha mazingira yake yanakuwa salama.
"Bahati nzuri maji hayana rangi kwamba mimi Simba au Yanga, hivyo watu wote chanzo cheti ni kimoja tunaomba haya maji tuyatunze kwa bidii zote kwa maendeleo yetu na maendeleo ya vizazi vijavyo,"amesema.
Naye Mkurugenzi wa bodi ya maji bonde la Wami/Ruvu Elibariki Mmassy eneo la Makutopora ndiyo linalolisha mkoa wa Dodoma hasa kwa upande wa maji na kusema kuwa changamoto kubwa katika eneo hilo ni ukataji wa miti, uchomaji mkaa na shughuli mbalimbali za kibinadam kwa watu wanao wanazunguka eneo hilo.
Amesema wanaendelea kuitoa licha ya kuwepo kwa wimbi kubwa la uchomaji wa moto eneo la hifadhi hasa kipindi hiki cha ukame ambapo u nahitajika moto mdogo sana na majani yanakuwa yameshika moto .
"Pia kuna wenyeviti ambao sio waaminifu ambao wamekuwa wakiuza mashamba bila kufata utaratibu, kwahiyo uharibifu upo lakini bodi ya mto Ruvu imekuwa na mikakati dhabiti kabisa kuhakikisha shughuli hizi zinasitisha na tunapunguza uharibifu katika chanzo chetu hiki,"amesema.