WAFANYABIASHARA WA CHUNYA WAILALAMIKIA SERIKALI YA AWAMU YA SITA.

MUUNGANO   MEDIA
0

Wafanyabiashara wa wilaya ya Chunya wailalamikia serikali kwa kukosa miundombinu Bora ya barabara Katika soka uhindini pamoja na ukosefu wa umeme na maji Katika soko ilo ambalo linapelekea ukose wa ufanyaji wa biashara na kupelekea anguko la kiuchumu Katika Wilaya hiyo.


Hayo yamebainishwa na wafanyabiashara wa wilaya hiyo wakati wa mkutano wa wafanyabiashara ulioongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Bw. Hamis Livembe September 7 Mwaka huu ikiwa lengo ni kupokea changamoto , kero na maoni ya biashara Ili kutafutiwa ufumbuzi.


 Mmoja wa wafanyabiashara wilayani hapo Qeen Mwasakela amesema kuwa tatizo la umeme Lina takribani Miaka kumi toka soko ilo kuaza kufanya kazi hivyo wanaiomba serikali kuhakikisha wanatatua kero hiyo.


Naye katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Mkoa wa Tanga Ismail Masoud amewataka wafanyabiashara waache tabia woga za kuogopa kusema kero zao Pindi wanapokabiliwa na changamoto.

" Nawashangaa Sana mfanyabiashara anaona Bora abaki na tatizo lake kwa kuogopa akisema atafanyiwa kitu kibaya wakati ndio anaongeza tatizo na kupelekea kushuka kwa biashara yake" amesema Ismaili Masoud.


Katika atua ingine Masoud amesema kuwa wafanyabiashara waache kuunga urafiki na maafisa TRA ambao wenye nia ovu na mpango wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais SAMIA Suluhu Hasani kwani maafisa hao ndio wanaoangusha juhudi za Rais Samia.


" Kitendo Cha mfanyabiashara kuungana na Afisa wa TRA Ili apunguziwe Kodi kitaendelea kumnyonya mfanyabiashara huyo kwani maafisa wengi huwa wanapokea rushwa ya kifedha kudai wanapunguza Kodi au kufutiwa kabisa ila baada ya Miaka kadhaa deni unalikuta vile vile" amesema Ismaili Masood.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania Bw. Hamis Livembe amesema kuwa kitendo Hiki Cha ukosefu wa huduma Bora za msingi za kibiashara zinapelekea kushuka kwa biashara na ukosefu wa ulipaji Kodi hivyo kama kiongozi atahakikisha changamoto hizi zimefikishwa kwenye mamlaka husika Ili kufanyiwa ufumbuzi.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)