Mch.Gervas Mbipi Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa Kisasa Jijini Dodoma
Na.Mwandishi Wetu Dodoma.
Imeelezwa
kuwa shule zinazomilikiwa na Kanisa la Waadventista Wasabato zimekuwa na mchango mkubwa wa kuwalea
na kuwajenga watoto katika maadili mema hasa katika ulimwengu huu uliopotea na
wenye mmomonyoko wa maadili kwa vijana.
Mch.Gervas Mbipi Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa Kisasa Jijini Dodoma akiwa katika ibada ya Sabato Kanisa la Waadventista Wasabato Chang'ombe Dodoma.
Hayo yamesemwa
na Mchungaji wa Kanisa la Waadventista Wasabato Mtaa wa Kisasa Jijini Dodoma
Mchungaji Gervas Mbipi katika ibaada ya
Sabato Kanisa la Wasabato Chang’ombe Dodoma iliyokwenda sambamba na changizo maalum
kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Iringa Adventist iliyopo Manispaa ya Iringa
ambapo makanisa yote ya jimbo la Kati mwa Tanzania(CTF) yamefanya changizo
maalum kwa ajili ya shule hiyo.
“Shule za
Kanisa la Waadventista Wasabato zimeanzishwa
kwa lengo maalum kuifanya jamii kuwa na maadili mema na kukabiliana na
mmomonyoko wa maadili katika jamii ,shule hizi ni kuwaweka sawa vijana kufanya
kazi na kutimiza wajibu wao na kuutangaza ufalme wa Yesu Kristo hivyo ni muhimu
kuziunga mkono shule zinawaandaa vijana
kuwa jamii bora inayopingana na rushwa,hofu ya Mungu na kuwa taifa bora”amesema.
Baadhi ya Kwaya zikishiriki katika huduma ya Uimbaji Kanisa la Waadventista Wasabato Chang'ombe Dodoma
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

