WAZIRI BASHE AZINDUA USAJILI KWA AJILI YA WASHIRIKI WA KONGAMANO LA USALAMA WA CHAKULA.

MUUNGANO   MEDIA
0

Waziri wa Kilimo, Mh Hussein Bashe amezindua rasmi usajili kwa ajili ya washiriki wa Kongamano la Usalama wa Chakula litakalofanyika Septemba 4-8 mwaka huu, jijini Dar es Salaam.


Pamoja na mambo mengine kongamano hilo litaangazia nafasi ya bara la Afrika katika matumizi ya mbinu bunifu zitakazohakikisha dunia inakuwa na chakula cha uhakika na salama.


Katika hotuba yake kabla ya kuzindua usajili huo, Waziri Bashe amewaalika wadau wa kilimo wakiwemo Wataalamu wa Masuala ya Mifumo ya Chakula Duniani, Waziri Bashe amesisitizia umuhimu na nafasi ya viongozi wa Afrika katika kuchangia uwepo wa Usalama wa Chakula kwa

ngazi za Taifa na Bara zima kwa ujumla huku akisisitizia uushiriki wa vijana na wanawake.


“Wakati tukiendelea na jitihada za kuliwezesha Bara la Afrika kuwa kitovu cha usalama wa chakula duniani, tunapaswa kuwapa kipaumbele vijana na wanawake katika harakati hizi kwa kutumia uwezo wao wa ubunifu na ufanyaji kazi unaoweza kuchangia maendeleo na uhakika wa

upatikanaji wa chakula cha uhakika na salama”.


Amesema kuwa mkutamo wa AGRF mwaka huu unafungua milango ya matumizi ya ubunifu katika kuimarisha kilimo pamoja na kufungua milango ya

uwekezaji zaidi itakayohakikisha uwepo wa ubunifu, utungwaji wa sera bora pamoja na uwekezaji kwenye sekta ya kilimo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa hilo, Bw. Amath Pathe Sene amebainisha kuwa Ubinifu, Sera Bora na Uwekezaji wa Kimkakati ni

njia sahihi katika kuhakikisha upatikanaji wa mifumo imara ya chakula.


Pia amesema Septemba 3, wageni wa mkutano huo watapata wasaha wa kutembelea na kujionea shughuli za kilimo zinazofanywa na watanzania na kujionea mafanikio mbalimbali yaliyofikiwa.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)