Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso (Mb) ametaka utafiti ufanyike zaidi ili kuweza kugundua mabonde mengi yatakayofaa kwa ajili ya uchimbaji wa visima vitakavyoongeza uzalishaji na upatikanaji wa huduma ya maji katika jiji la Dodoma.
Amesema Jiji hilo kwa sasa uhitaji wa maji ni lita za ujazo mil 133.
Waziri Aweso ameyasema hayo akikagua mradi wa maji wa Nzuguni ambapo amepokea mabomba yatakayotumika katika kusambaza maji maeneo ya Nzuguni,Ilazo ,Swaswa na viunga vya jirani, hadi sasa visima vilivyo chimbwa katika eneo hilo ni visima 5 vyenye uwezo wa kuzalisha lita mil 7 kwa siku.
Mradi huo ukikamilika utaweza kuwanufaisha zaidi ya wananchi 75,000.
