TUCTA yaomba serikal kupunguza viwango vya kodi katika mishahara.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na Emmanuel Kawau.

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Nchini (TUCTA) imeipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu kwa jitihada zake za kuboresha maslai ya wafanyakazi kwa kuongeza viwango vya mishahara kila mwaka.


Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam Naibu katibu mkuu wa TUCTA Said Wamba amesema licha ya kuongezwa kwa nyongeza za mishahara bado kunachangamoto mbalimbali kwa wafanyakazi ikiwemo kodi kubwa katika mishahara,mikataba ya hali bora ya wafanyakazi wa umma.


Ameongeza kuwa Wanaiomba serikali kutazama upya viwango vya kodi katika  Mishahara ya wafanyakazi ikiwa ni pamoja na sheria zake ili nyongeza za msharaha ulete tija kwa wafanyakazi kwa kuwa na maslai mapana yatakayochochea ufanisi kazini.


"Moja ya matatizo makubwa kwa wafanyakazi katika nchi yetu na nchi nyingi ni kodi kubwa,watu wanatozwa kodi karibu katika kila kitu wanachofanya hasa wafanyakazi, wafanyakazi hawawezi kukwepa kulipa kodi kwasababu mishahara yao na kipato chao kinajulikana". Alisema Wamba.


Wamba amesisitiza kuwa Vyama vya Wafanyakazi sio vyama vya mapambano bali ni vyombo vya majadiliano ambavyo vinapaswa kuwa mstari wa mbele kuandaa ajenda kwa maslai ya wanachama wake mapambano yanatumika pale majadiliano yanaposhindikana.


Aidha amewataka wafanyakazi Nchini kufanyakazi kwa bidii ili kuongeza nguvu katika kudai nyongeza za mishahara ikiwa ni pamoja na kizingatia muda wa kufanyakazi.

"Haitoshi kudai nyongeza ya mishahara,ni lazima mishahara tunayodai  itokane na tija ya utendaji katika sehemu zetu za kazi".

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)