MILIONI 500 ZATENGWA KUENDEZA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA BAGAMOYO.

MUUNGANO   MEDIA
0

Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deogratius J. Ndejembi amesema katika mwaka wa fedha wa 2023/24 Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imetenga shilingi milioni 500 kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa jengo jipya la Utawala.

Ameeleza hayo wakati alijibu Swali la Mhe. Muharami Shabani Mkenge, Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo, aliyetaka kujua Je, ni lini Serikali itajenga jengo jipya la Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Ndejembi amesema Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo ipo katika maandalizi ya kuanza ujenzi wa Jengo hilo kupitia fedha za Mapato ya Ndani ya Halmashauri ambapo katika mwaka wa Fedha wa 2022/23 jumla ya shilingi milioni 500 zimetengwa.

Aidha, Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo imekamilisha maandalizi ya nyaraka za ujenzi wa jengo hilo na kuwasilisha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuidhinishwa ili ujenzi uweze kuanza kwa kuwa Halmashauri hiyo imepanga kutumia mchoro wao badala ya mchoro ulioandaliwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Ndejembi amesema Serikali inatambua uhitaji wa Jengo jipya la Utawala katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)