Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam *CPA, Amos Makalla* ameelekeza Jukwaa la uwekezaji Wanawake kiuchumi Mkoa huo kuja na *mpangokazi wa kuleta mabadiliko chanya kwa Wanawake* ikiwa ni pamoja na kuwafikia wengi zaidi Ili *kuleta tija na mabadiliko ya kiuchumi.
*RC Makalla* ametoa maelekezo hayo wakati *ufunguzi wa Mafunzo maalumu kwa Viongozi wa majukwaa ya Wanawake* Mkoani humo ambapo ameelekeza mafunzo waliyopata wakayashushe *ngazi ya Wilaya, Kata na mitaa Ili kunufaisha Wanawake wengi zaidi.*
Aidha *CPA,Makalla* ameelekeza *dhana ya uwezeshaji Wanawake kiuchumi iende sambamba na kuwapatia fursa* mbalimbali zinazopatikana Ili kuwakwamua kiuchumi.
Pamoja na hayo *RC Makalla* amesema mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa *agizo la Rais Dkt, Samia Suluhu Hassan* alilotoa kwa Kila Mkoa *kuyalea na kuyatunza Majukwaa ya Wanawake.
Sanjari na hayo *CPA, Makalla* amewataka Viongozi wa majukwaa ya Wanawake *kuelimisha Wanawake* Kuhusu umuhimu wa *kufanya mambo machache kwa ufanisi na tija* na sio kujaribu Kila biashara.
