IDADI YA WAHANGA WA MAFURIKO NA MAPOROMOKO YA UDONGO RWANDA YAFIKIA 136.

MUUNGANO   MEDIA
0

Idadi ya watu waliofariki dunia nchini Rwanda kufuatia mafuriko na maporomoko ya udongo yaliyoyakumba baadhi ya maeneo ya nchi hiyo imeongezeka na kufikia 130.

Shughuli za mazishi zimekuwa zikifanyika katika maeneo tofauti yaliyokumbwa na mafuriko nchini Rwanda.

Katika mji Wa Rubavu watu 13 wamezikwa leo katika kabiri la Rugerero na kuhudhuriwa na wakuu wa serikali akiwemo waziri mkuu Edouard Ngirente.

Serikali inasema hadi sasa watu wasiopungua 130 wamefariki kutokana na mafuriko yaliyotikisa majimbo ya magharibi na kaskazini mwa Rwanda.

Jimbo la Magharibi - na kaskazini mwa Rwanda - ni maeneo yenye milima ambayo mara nyingi huathiriwa na maporomoko ya ardhi wakati wa misimu ya mvua.

Nayo Wizara ya Maafa iliwatahadharisha wananchi kuwa waangalifu mnamo wakati huu. Mvua kubwa ilinyesha katika maeneo tofauti nchini Rwanda jana usiku, idadi ya uharibifu na vifo inatarajiwa kuongezeka.

Taarifa zaidi zinasema, "Barabara nyingi zimeharibika kwa kukatika na kufunikwa na matope hivyo sasa ni vigumu kupitika".

Nchini Uganda, ripoti zinasema vijiji kadhaa vilisombwa na mafuriko kufuatia mvua kubwa ya hivi karibuni katika kanda hiyo huku watu wanane wakiripotiwa kuaga dunia.

Kwa mujibu wa shirika la Msalaba Mwekundu la Uganda wengi wa waliokufa ni wanawake na watoto.

Uganda kama ilivyo katika mataifa mengine ya Afrika Mashariki imekuwa na mvua kubwa. Meneja wa mawasilinao wa shirika la Msalaba Mwekundu Uganda amesema juhudi za kuwasaidia walioathirika zinaendelea.

Chanzo #Parstoday.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)