MWAKATA, SUNGAMILE KUPATIWA HUDUMA YA MAJI ZIWA VICTORIA-AWESO.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Na.Mwandishi wetu Dodoma.

Waziri wa Maji Juma Aweso amesema Serikali inafanya tathmini upya kuhakikisha Vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi mkubwa wa Maji ya bomba kutoka Ziwa Viktoria ikiwemo vijiji vya kata ya Mwakata na   Kijii Cha  Sungamile vinapata huduma hiyo .

Mhe.Aweso amebainisha hayo leo Mei ,2,2023 wakati akijibu swali la nyongeza za Mbunge wa Msalala Mhe.Idd Kassim aliyehoji ni lini Serikali itahakikisha vijiji vyote vilivyopitiwa na mradi wa Maji kutoka Ziwa Viktoria vinanufaika na huduma ya Maji ikiwemo Mwakata na Sungamile.

Akijibu swali Waziri Aweso amesema mpango wa Serikali ni kufanya tathmini upya kuhakikisha Vijiji vyote vilivyokosa huduma ya kupitishiwa Maji licha ya kuwa na fursa ya kupita mradi mkubwa huo wa Maji.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)