Soko la fedha la dunia lipo katika wakati usiotarajika Wala kupimika mwenendo wa kesho yake kutokana na migogoro ya siasa za kimaeneo na kiuchumi zinazo endelea Sasa.
Mataifa mengi ya ulimwengu wa pili na wa kwanza yapo katika migogoro ya kiuchumi na siasa za kimaeneo (geopolitics) ambapo madhara yake Yana athari katika chumi za mataifa ya dunia ya tatu.
Hivyo basi inapelekea kuwa na soko la fedha lisilopimika kesho yake mataifa mengi yanajihami kwa kuweka akiba zao katika dhahabu kulinda utajiri wao mfano taifa la China linaongoza kwa kuwa mteja mkubwa wa dhahabu kwa mjibu wa tasisi inayosimamia biashara ya dhahabu duniani China mpaka March 2023 imenunua tani 103 za dhahabu ikifuatiwa na Urusi iliyonunua tani 31 na India tani 2.8.
Kwanini mataifa mengi yananunua dhahabu Kama akiba yao ya fedha za kigeni jibu ni kwamba dhahabu inathamani ya ndani pia uhitaji wake kidunia hauna ukomo tekinolojia ya anga na vifaa vya kielekitroniki vinauhitaji mkubwa wa dhahabu hivyo ina uthamani wa ndani yaani (intrisic value) kuzidi fedha katika mfumo wa makaratasi ambazo zikiacha kutumika hazina uthamani wowote wa ndani.
Mataifa mengi ya ulimwengu wa pili na watatu yameanza kuweka akiba ya fedha za kigeni katika thamani ya dhahabu kwa wingi
Taifa letu pia mwaka Jana Mhe.Rais Dr.Samia Suluhu hassani aliweza kusisitiza benki ya taifa kuandaa utaratibu wa kununua dhahabu kama akiba yake ya fedha za kigeni mpaka Sasa wamenunua KG400 za dhahabu.
Umhimu wa fedha za kigeni au akiba ya fedha za kigeni husaidia taifa katika utawala na usimamizi wa sera za kiuchumi na sera za kifedha pia hutumika Kama amana katika mikopo ya serikali kwahivyo Ni mhimu na Ni utaratibu na ni sheria mataifa yote yaliyo katika jumuiya ya madola kuwa na akiba ya fedha za kigeni kwa mjibu wa sheria ya akiba za benki kuu ya umoja wa mataifa 1952 (federal Reserve Act 1952).
Banki ya taifa lolote inahitajika kuwa na kiwango Fulani Cha akiba ya fedha za kigeni,Maranyingi akiba hizo huwa na kiwango maalumu ambapo chini ya kiwango hicho Cha akiba basi taifa linaweza kutangaza Hali ya hatari Kama Kama akiba haiwezi kuhimiri uchumi wa nchi husika.
Mataifa yanayo ongoza kwa kuwa na akiba ya fedha za kigeni katika dhahabu Ni Marekani,Germany,Italy,France mfano marekani ina akiba ya tani 8100 za dhahabu katika akiba yake ya fedha za kigeni ikifuatiwa na maifa mengine.
Soko la fedha la kidunia lipo katika hatua ya ushindani ambapo mataifa ya ulimwengu wa pili na watatu yapo katika njia panda aidha kuendelea kuweka akiba kubwa ya fedha za kigeni katika dola au dhahabu kujihami na mazingira yasiyo kuwa na makisio ya soko la fedha la dunia kutokana na migogoro ya siasa za kimaeneo na kiuchumi.
Imeandaliwa na Joel Kasasa, Mwalimu na mchambuzi wa masuala ya kiuchumi.