Na Emmanuel Kawau.
Chama cha ACT -WAZALENDO kupitia kwa waziri wake kivuli wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi wameishauri Serikal kuhakikisha inatekeleza miradi ya maendeleo kwa wakati ili kuepuka ongezeko la gharama,kudhibiti ubadhilifu wa fedha za umma ikiwa ni pamoja na kusimami maslai ya madereva wa masafa marefu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati akiwasilisha Uchambuzi wa Bajeti ya Ujenzi na Uchukuzi kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Waziri Kuvuli wa Miundombinu ya Ujenzi, Reli na Barabara Eng. Mohammed Mtambo Amesema ,kuna ucheleweshaji wa ukamilishaji wa mradi. Kipande cha kwanza na cha pili vipo vyuma
ya wakati kwa zaidi ya miaka mitatu.Hali ya utekelezaji wamradi huu kwa mujibu wa ripoti ya hali ya uchumi nautekelezaji wa bajeti wa Wizara ya Fedha kwa mwaka 2023/24 hadi kufikia
Juni 2023 hakuna kipande hata kimoja kilichokamilia.
"Hali halisi inaonyesha kuwa; kipande cha Dar es Salaam –Morogoro kimekamilika kwa asilimia (97.65 %), Morogoro –Makutupora (91.32%), Mwanza –Isaka (19.70%) Makutupora –Tabora (3.26%);Hata hivyo mradi huo uliongezwa muda wa kukamilika mara saba sawa na miaka 3.8.Ila hadi sasa bado ujenzi haujakamilika kwa muda uliopangwa Hii imepeleke kuongezeka kwa gharama ya zaidi ya
Shilingi bilioni 25" Alisema Mtambo
Pili,kuongezekakwa gharama ya Ununuzi wa treni (vichwa vya treni, treni za kisasa za umeme
na mabehewa ya abiria).
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabuza Serikali ameibua hoja ya ukiukwaji wa sheria ya
manunuzi na hivyo kupelekea kuongezeka kwa gharama za manunuzi. CAG anasema kuwa
Gharama ya Ununuzi wa treni (vichwa vya treni, treni za kisasa za umeme na mabehewa ya
abiria) iliongezeka kwa Dola za Kimarekani milioni 215 baada ya kukataliwa kwa zabuni zingine
zote bila sababu ya msingi.
Katika swala lingine ACT imeonyesha wasisi wake juu ya ubia wa sekta ya umma na binafai (PPPs) na kuuita "Zimwi" huku ukionekana kuzidi kukuzwa kama njia ya kupata fedha
zinazohitajika ili kutekeleza miradi ya maendeleo hususani ujenzi wa miundombinu ya reli na Barabara ambapo katika bajeti ya wizara ya mwaka 2023/24 umeonekana kutawala zaidi kwenye mradi wa reli ya Mtwara –Mbambabay na matawi yake ya Liganga na Mchuchuma na Tanga–Arusha –Musoma,Barabara ya Chalinze hadi Morogoro kujengwa kwa mfumo huo.
"Hoja inayojengwa ni kwamba ubia wa sekta ya umma na binafsi unapotumika kwenye ujenzi wa miundombinu unapanua wigo wa muda wa kulipia kutoka papo kwa papo hadi muda mrefu zaidi masikitiko yetu makubwa na tahadhari tunayoitoa kwa Serikali kutokumbatia mwelekeo huu kwa kuwa hoja zinazojengwa zinajaribu kupumbaza umma kama ni njia ya kujikomboa kumbe unawapeleka kwenye utumwa kwa kuongeza mzigo na minyonyoro kwa walipa kodi. Pia, Ubia (PPP) mara nyingi ni ghali zaidi kutokana na gharama ya mtaji, matarajio ya faida ya makampuni binafsi na gharama za malipo ili kujadili mikataba tata ya Ubia (PPP)."Amesema Mohammed.
Kadhilika Mtambo amezungumzia uwekezaji na hasara katika uendeshaji na usimamizi wa Ndege za Shirika la ATCL,hasara inayopata ATCL kwa sehemu kubwa inatokana na mfumo wa umiliki wa ndege.Mfumo uliopo sasa ATCL haimiliki ndege. Ndege zote
zilizonunuliwa na Serikali kwa fedha za walipa kodi zinamilikiwa na Wakala wa ndege za Serikali TGFA na kukodishwa kwa ATCL. Mfumo huu unaoleta hasara kwa taifa unatokana na uamuzi wa mwaka 2016.
Aidha katika uchambuzi wa Waziri kivuli huyo amezungumzia swala la msongamano Bandari ya Dar es Salaam ambapo amesema
Kwa muda mrefu kumekuwa na malalamiko yasiyoisha ya kuwepo kwa msongamano wa magari unaopelekea kuwepo kwa muda mrefu wa kusubiri kupakia au kupaku mizigo,ucheleweshwaji unaosababisha na uwezo wa bandari kumudu mahitaji hayo, unapaswa kufanyiwa kazi kwa
haraka. Hususani katika kipindi hiki ambapo gharama za vitu vimekuwa juu, gharama zinazoweza kuokolewa kwa kuboresha utendaji na uwezo wa bandari zitaenda kuwasaidia wananchi kupata huduma kwa bei ya chini kuliko hivi sasa.
Pia ACT inaitaka serikali kusimamia Madai na stahiki za madereva wa masafa marefu ambao
Kwa muda mrefu madereva wa magari ya masafa marefu (Nje ya Nchi) wamekuwa na
malalamiko yasiyosikilizwa kuhusu maslahi yao, mazingira yakazi na mifumo ya sheria na
utekelezaji wake katika kusimamia madereva na sekta ya usafirishaji.
" Mambo yanayolalamikiwa
sana yakihusisha; matamko ya mara kwa mara ya uendelezaji wa mafunzo au ujuzi wa udereva. Madereva wamekuwa ni waathirikawa kuanzishiwa operesheni maalumuza kuendeleza ujuzi kwa gharama zao bila ya kuwa na mfumo shirikishi ACT tunaitaka Serikali kusimamia utekelezaji wa sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka
2004 katika sekta ya usafirishaji (madereva).
Pili,tunataka Madereva wanaosafirisha nje ya nchi walipwe malipo mazuri tunapendekeza
walipwe kwa Viwango vya Kimataifa kama wanavyolipwa madereva wa nchi wanachama wa
Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini Afrika SADC"
ACT Wazalendo wameitaka Serikali kushughulikia masuala ya utengezaji wa vivuko na meli kwa
umakini na uharaka. Meli na vivuko hivyo virudi kufanya kazi ili kusaidia kuondoa adha kwa watumiaji wa vivuko hivyo.
Pili, tunaitakaTaasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) kuchunguza upya mchakato wa zabuni ya MV KIGAMBONI kwani kuna mashaka kwa Umma kwamba
matengenezo yake yana viashiria vya rushwa na upendeleo.
Aidha tunatoa wito kwa Serikali kuwekeza vizuri kwenye kuboresha miundombinu ya vivuko na
kuwachukulia hatua kali za kisheria wote wanaohujumu miundombinu. Serikali iachane na
mawazo yoyote ya kubinafsisha huduma ya vivuko,Pia wameitaka kushughulikia Ucheleweshaji wa Miradi ya Barabara maeneo ya pembezoni.
