Tuzo za Harusi kufanyika mei 28 mwaka huu.

MUUNGANO   MEDIA
0

Na Emmanuel Kawau.


Tuzo za harusi awamu ya tatu zinatarajiwa kufanyika katika hotel ya Hyatt regency Jijini Dar es salaam kuanzia saa moja na nusu usiku siku ya Tarehe 28/05/2023.



Akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya waandaaji wa hafla hiyo Benedict Msofe amesema tuzo hizo zinakusudia kutambua na kusherehekea jukumu muhimu linalofanywa na wachuuzi wa harusi,wauzaji na watoa huduma kwa kufanya siku za harusi kuwa maalumu,za kupendeza na za kukumbukwa.


"Imekuwa miaka minne tangu tulipofanya maonyesho ya biashara ya harusi na kulingana na mafanikio makubwa ya maonyesho hayo yaliyofanyika hapo awali na maoni mazuri kutoka kwa wadau mbalimbali waliohudhuria tulifikiria kwamba ni wakati muafaka wa kuanzisha tuzo za harusi ambazo zitafanyika kila mwaka.......na mwaka huu ikiwa ni mwaka wetu wa tatu kusherehekea tuzo hizo" Amesema Msofe.


Ameongeza kuwa kwa miaka michache iliyopita sekta ya harusi imekuwa na kugeuka kuwa biashara rasmi ambapo kwa wastani sherehe 350 za harusi hufanyika  jijini Dar es salaam,hivyo kutoa fursa za ajira kwa watanzania.


Aidha Msofe ameyataja makundi ya tuzo yanayowaniwa ambayo yapo 19 katika kipindi cha mwaka mmoja ambayo ni; ukumbi bora wa harusi,mwokaji bora wa keki,mtaalamu wa maua,mpiga picha bora,mchukua video bora,mpangaji bora wa matukio ya harusi,mpishi bora wa harusi,mtengeneza vitafunwa bora,mtengeneza nywele  na mwanamitindo bora,salon bora,mshereheshaji bora (MC).


Makundi mengine ni pamoja na Dj bora,,muuza vifaa vya harusi,duka la vifaa vya harusi,duka la nguo za maharusi wakike,muuza vito vya harusi,mchoraji bora wa henna,mbunifu wa nguo za kiume,tuzo za heshima hutolewa kwa harusi bora ya mwaka na tuzo ya mafanikio kwa mtu binafsi/taasisi iliyoacha alama kwenye sekta ya harusi.


Kwa upande wake Miss Bahiya Tajiri kutoka innovex Tanzania amesema kwa takribani miaka miwili mfululizo wamekuwa wakishirikiana na Tuzo za Harusi kuhakikisha ubora wa kura na wanaamini tuzo hizo zinatija kubwa katika jamii pia amewahakikishia wananchi kuwa kura zitakuwa huru na za haki.

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)