Emmanuel Kawau.
Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya umefanya utafiti katika Sekta isiyo rasmi ili kubaini mtazamo wa jamii kuhusu bima ya afya kwa wote wananchi ambapo matokeo yanaonesha asilimia 86 ya watu kutokuwepo katika mfumo wa bima ya afya.
Akizungumza katika warsha ya uwasilishaji wa matokeo ya utafiti jijini Dar es Salaam, Afisa Miradi kutoka Ubalozi wa Uswiss nchini Jacqueline Matoro, wanatumaini matokeo hayo yatakuwa msingi wa mazungumzo zaidi ya kiufundi yatakayochangia katika uundaji wa sera bora ya bima ya afya kwa wote.
Ameongeza kuwa Warsha hiyo pia imelenga kuwashirikisha watafiti, watunga sera, watoa bima, na mdhibiti wa bima kuhusu matokeo ya utafiti wa kisayansi na mapendekezo kuhusu namna Bima ya Afya ya CHF Iliyoboreshwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya (NHIF) inavyoweza kuchangia katika uundwaji wa sheria ya Bima ya Afya kwa wote.
Kwa upande wake Mratibu wa Bima ya Afya Taifa kutoka Ofisi ya Rais Tawala Mikoa na Tawala za Mitaa (TAMISEMI) Silvery Maganza amesema bima ya afya ya CHF imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na mifumo inayosaidia wananchi waweze kupata huduma za afya.
Aidha amesema kuwa ili kufikia bima ya afya kwa wote wanapendekeza kuwa na mifumo rafiki ya usajili wa wananchama kutokana na uzoefu walioupata katika CHF iliyoboreshwa, kutokuwa na mfumo mzuri wa usajili kutasababisha kutumia muda mrefu katika kupata wanachama.
Pia amesema kuwa kuwepo na gharama nafuu za uchangiaji katika mfuko huo ili kila mwananchi aweze kuufikia ikiwa ni pamoja na kuwa na kuwa na mfuko himilivu na kuhakikisha wakati wote unakuwa na fedha katika kuondoa usumbufu wa wananchi kukosa huduma za afya,
Nae Meneja Mradi wa HPSS Ally Kebby amesemaTafti hizo zilizofanyika zinatoa majibu ambayo yanaweza kukidhi makundi yote ya wananchi katika jamii,waliojialijili na waajiliwa wote kuweza kumudu gharama za bima ya afya kwa wote.
Mradi wa HPSS Tuimarishe Afya unafadhiliwa na Serikali ya Uswisi kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.


