February 24,2022 Urusi iliivamia rasimi kijeshi Ukraine ikitaka kuyakomboa majimbo manne Donetsk,kherson,luhansk na zaporizhia oblasts.
Katika nyakati tofauti mataifa G7 na umoja wa ulaya na washirika wake walianza kuiwekea Urusi Vikwazo vya kiuchumi kwa awamu tofauti ikiwa Ni pamoja na kutaifisha Mali za Russia kwenye nchi zao na kufunga akaunti za Urusi kwenye mataifa yao kwa Zaidi ya Euro billion 150 za Urusi zilipotelea kwenye Vikwazo hivo.
Vikwazo vya US na Umoja wa ulaya vimepelekea kuibuka kwa wimbi jipya la mataifa ya ulimwengu wa pili kutaka kuachana na Dollar na kutafuta fedha mbadala katika biashara ya kimataifa kwani mda wowote marekani na Umoja wa ulaya vinaweza kutumia umiliki wao wa soko la fedha kuyumbisha au kuzolotesha uchumi wa nchi yoyote.
Mfano Vikwazo vya USA kwa Iran kutokana na kuipatia Urusi Drones za kivita na Vikwazo vya kuizuia China kutumia semiconductor kwa maana ya microchips kwenye teknolojia yao ya kijeshi viliibua hisia mpya za mataifa haya kuona namna gani wanaweza kujihami na nguvu ya Dolla.
Mfano microchips zinazotumika kwenye simu,komputa(tanakilishi) na servers nyingi zinategemea semiconductors udhitibi wa mojakwa moja wa US kwenye usambasaji na usalishaji wa hizi semiconductor ni tishio kwa uchumi wa China ambao unategemea na ni mteja mkubwa wa bidhaa hizo.
Udhitibi na vikwazo vya USA kwa kampuni ya ZTE ya China iliipa China tahadhari kubwa kwani kampuni ya ZTE ilikuwa inaingiza pato la Dolla billion 16 kwa mwaka ikiwa na staff 70,000 elfu waliopoteza vibarua silicon chips Ni mhimu kwa uhai wa teknolojia ya dunia mpya (modern world technology) kutoka kwenye artificial intelligence kwenda kwenye cyber security and 5G China inatumia Dolla billion 200 kwa mwaka kuagiza semiconductors.
ZTE ni kampuni kubwa ya kutengeneza simu ya China inayotegemea microchips siliconi zinazozalishwa Taiwan na Korea kusini ambazo pia hutegemea baadhi ya malighafi mhimu marekani kwajili ya kutengeneza smartphone nzuri zenye Kasi ya mtandao.
Mataifa yanayozalisha chips hizo Ni Kama Korea kusini, Taiwan na USA Kama supplier ya baadhi ya materil mhimu japo viwanda vipo Korea kusini na taiwani.
Mataifa ya ulimwengu wa pili na tatu yanapambana kuacha kutegemea Dolla kwa hofu ya namna ambavyo USA kwa mda wowote inaweza kutumia Dolla Kama fimbo.
Iran na Russia walianzisha mchakato wa kuunganisha mawasiliano ya kibenki (interbank communication SPSF) kama mbadala wa SWIFT ni jitihada angalau za kuonesha mwanga kwa nchi zingine kwani Vikwazo vya kiuchumi kwa Urusi vimeyapa mataifa mengine tahadhari.
Mataifa yaliyo kenye umoja wa BRICS Yanachukua tahadhari kwa kununua dhahabu kwa wingi kuweka kwenye hazina zao badala ya Dolla China inashusha thaman Yuan ilikukuza uhitaji wa bidhaa zake kwenye soko la dunia hatua hii inapelekea mataifa mengine angalau kwa kiasi fulani kuhitaji reserve ya Yuan ku settle payments na China kwenye soko la dunia.
Mwaka 2014 baada ya Urusi kuvamia Ukraine na kuchukua Jimbo la Crimea ilitishiwa kuondolewa kwenye mfumo wa mawasiliano ya kibenki kimataifa wa SWIFT payments ambapo ilianza kujiandaa taratibu kujihami na kikwazo hicho na kuanzishwa mfumo wao wa SPSF ambao aliunganisha na Iran mwaka 2018.
Iran ilianza pia kujihami mapema tangu 2015/2018 kutokana na dili la nuclear ambalo USA aliingia kupinga chumi za Iran na Urusi zinategemea bidhaa za Aina moja hivyo kuunganisha mfumo wa SWIFT kwa hatua ya swali kunaweza kukosa meno kwa USA lakini mwitikio wa mataifa mengi ya ulimwengu wa pili na wa tatu kuachana na dola wanaweza kupata wateja wengi Zaidi na kufaulu kwa asilimia kubwa.
Mataifa yanayounda BRICS hayana historia ya kikoloni na mataifa mengi ya dunia ya tatu pia sera zao za Mambo ya kigeni za kutoingilia Mambo ya ndani ya mataifa wanachama yanaleta mvuto mkubwa kwa mataifa mengi Zaidi kujiunga bado Vita hii ya kiuchumi haina tahmini ya moja kwamoja ya kutoa ushindi kwa aidha Urusi na China dhidi ya mataifa ya G7 na USA.
Imeandaliwa na Joel Kasasa Dodoma, 0782392694.