MAJAMBAZI WANNE WAUWAWA WAKITEKELEZA TUKIO LA UNYANG'ANYI DODOMA.

MUUNGANO   MEDIA
0

 

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma limefanikiwa kuwathibiti majambazi wanne wa kiume ambao majina yao bado hayajatambulika wenye umri kati ya 25-30 waliokuwa katika harakati za kufanya tukio la unyang'anyi wa kutumia silaha tarehe 25/4/2023 majira ya saa 03:10 usiku mtaa wa Mwangaza, Kisasa Kata ya Dodoma Makulu.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 26,2023 na  Kamanda mkuu wa Jeshi la polisi mkoa wa Dodoma Martine Otieno wakati akizungumza na wandishi wa habari.

Kamanda Otieno amesema majambazi hao walivamia nyumbani kwa Bi. Edna Joseph Kashashari (41), mfanyabiashara, mkazi wa Kisasa wakiwa wamevaa barakoa usoni na kufanikiwa kunyang'anya pesa taslim 1,100,000/= simu ya Samsung moja na simu ndogo tatu baada ya watu hao kumtishia kumkata mapanga ndipo mhanga alipiga kelele za kuomba msaada.

“Baada ya mhanga kupiga kelele za kuomba msaada ambazo zilisikika kwa majirani na majirani hao kutoa taarifa kwa askari wa waliokuwa doria eneo hilo ambao walifika kwa haraka na kuwakuta watu hao ambao walijihami kwa kutaka kuwashambulia askari kwa mapanga na askari hao kujibu mapigo kwa kuwafyatulia risasi ambazo ziliwajeruhi watuhumiwa hao maeneo mbalimbali ya miili yao,”amesema.

Aidha ameongeza kuwa majambazi hao walijificha nyuma ya ukuta wa fensi na kuruka ukuta huo na kwenda kumvizia Edna Joseph Kashashari wakati anataka kufunga mlango wa nyumba na kumtishia kumkata na mapanga kisha kumpora vitu hivyo.

Amesema majambazi hao wanne walifariki dunia wakiwa wanapelekwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa matibabu.

“Kwasasa hali ya mkoa ni shwari na jeshi la polisi lipo makini kuhakikisha hali ya amani inaendelea kuwepo,”ameongeza.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)