Na Makunga Peter Makunga.
GEITA.
HALMASHAURI ya Mbogwe Mkoa wa Geita imepokea Pikipiki 6 kati ya 17 na kuwagawia Watendaji Kata ili kuwarahisishia kazi hasa za ukusanyaji wa mapato.
Habari kamili na Makunga Peter Makunga Kutoka Wilayani Mbogwe.
Hafla hiyo fupi ya kupokea na kuwakabidhi pikipiki watendaji kata limefanyika katika viwanja vya Halamashauri ya Mbogwe iliyoko kijiji cha kasosobe Bwelwa .
Pikipiki hizo zimetoka kwa Rais Dkt Samia suluhu hasani kupitia kwa mbunge wa viti maalumu Rose Busiga .
Awali ya yote kaimu mkurugenzi mteji wa halmashauri ya mbogwe Egidius Kahendaguza amesema pikipiki hizo zitarahisisha katika shughuli za maendeleo kwa watumishi hao.
Rose Busiga mbunge viti maalum amewakabidhi pikpiki na kuwaasa wazitunze.
Naye Polisi kata ya Mbogwe mkaguzi msaidizi INP DENIS RWEHUMBIZA kwa Niaba ya mkuu wa Polisi wilaya SSP Alex Mkonda amewataka watendaji kata hao wawe na leseni ya Udereva.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

