SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YAUNGA MKONO JITIHADA ZINAZOCHUKULIWA NA JUMUIYA YA KUHIFADHI QUR-AN TANZANIA KATIKA KUWAFINYANGA VIJANA.

MUUNGANO   MEDIA
0

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaunga mkono jitihada zinazochukuliwa na Jumuiya ya kuhifadhisha Qur-an Tanzania katika kuwafinyanga vijana ambao ndio nguvu kazi ya Taifa la Sasa na baadae.

Hayo yamesemwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe.Hemed Suleiman Abdulla katika Uzinduzi wa Tunzo ya Kimataifa ya Qur-an tukufu Tanzania 2023 uliofanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNICC)  jijini Dar es Salaam.

Amesema suala la kuwahifadhisha Qur-an vijana kutoka ndani na nje ya Tanzania pamoja na kutoa Tunzo katika mashindano hayo kunahitaji Imani, subra,uvumilivu,uthubutu na uchamungu wa hali ya juu kuweza kulifanikisha suala hili.

Mhe. Hemed ameupongeza uongozi wa jumuiya ya kuhifadhisha Qur-an Tanzania kwa kujitolea katika kusimamia harakati za kukiendeza kitabu kitukufu cha Qur-an kwa mustakbali mzima wa vizazi vya Sasa na baadae ambapo vijana hao wataisadia serikali kupata vijana wenye maadili na utumishi wenye nidhamu na hofu ya mungu.

Sambamba na hayo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametoa wito kwa jumuiya nyengine ambazo Zina mnasaba na utoaji wa elimu kuzingatia maadili ya dini pamoja na sera ya nchi katika mitaala ya elimu zinazotolewa ili kuepusha migogoro inayoweza kujitokeza na kupelekea sintofahamu ndani ya nchi. 

Katika kuelekea mwezi mtukufu wa Ramadhan Mhe.Hemed amewakumbusha wananchi wote na waumini wa Dini ya kiislamu kuendelea kudumisha ibada na kuacha maasi yote yaliyokatazwa na Allah S.W kwa kumcha M/Mungu kikweli,kutoa sadaka,kuwahudumia mayatima,kuwalisha masikini na kufanya Yale yote yanayompendeza M/Mungu na Mtume Muhammad S.A.W.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya ya kuhifadhisha Qur-an Tanzania Sheikh Othman Ali Kaporo Amaesema malengo makuu ya mashindano haya ni kukuenzi kitabu kitukufu cha Qur-an ili kumkinga mwanadamu kwa maovu na machafu ili kufika malengo ya serikali iliyojiwekea.

Katika hafla hio viongozi hao wa dini wamempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza miaka miwili ya Uongozi pamoja na kumuombea Dua ili aweze kuwatumikia watanzania.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)