TAASISI ZA UMMA NCHINI ZATAKIWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA KANUNI ZA SERIKALI MTANDAO.

MUUNGANO   MEDIA
0

 


Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya utumishi  wa umma na utawala bora ,Mhe. Jenista Mhagama  amezitaka Taasisi zote za umma  nchini kuhakikisha zinazingatia  na kufuata sheria, na kanuni za  Serikali Mtandao.

Ameyasema hayo Feb 10 jijini Arusha wakati akifunga  kikao kazi cha 3 cha Serikali mtandao kilichowashirikisha  zaidi ya watumishi wa umma 1600 kutoka mikoa mbalimbali nchini. 

Amesema kuwa,ni lazima taasisi zote za umma zihakikishe zinafuata sheria zilizopo ili kuwezesha kufanya kazi kwa weledi na uzalendo kwa ustawi wa nchi  na kuweza kuokoa gharama  kupitia huduma za kidigitali. 

“Naagiza mkaanze kufanya vikao vya kitaasisi  kila mwaka katika ngazi za wilaya na mkoa katika kuhakikisha mnatathimini huduma ya serikali mtandao katika ngazi za wilaya na mkoa ili huduma hiyo iweze kuboreshwa  na kutumia na taasisi zote za umma.”amesema  Waziri Jenista .

Aidha amewataka kupitia kikao hicho wakatekeleze  maazimio  yote  waliyojiwekea huku akiwataka kuendana na mabadiliko  ya kasi ya duniani ya teknolojia yaliyopo hivi sasa kwani hawatakiwi  kuwa nyuma .

“Wataalamu na wakuu wa idara  nawaomba sana mhakikishe  mnafanya  kazi zenu  kwa weledi na uzalendo mkubwa kwa faida ya Taifa letu, huku  mkihakikisha  kila mmoja anakuwa  mwaminifu  katika usimamizi wa  mifumo ya Tehama. “amesema Waziri Mgahama.

Kwa upande wake Mmoja wa washiriki katika mkutano huo,ambaye ni Katibu Tawala wa mkoa wa  Njombe ,Judica Omary amesema kuwa,kikao hicho ni cha tatu kufanyika na wameweza kujadili changamoto  mbalimbali na kuweka mikakati na  maboresho mbalimbali ikiwemo ya  kuongeza matumizi ya mtandao serikali. 

Amesema kuwa, kikao hicho kimekuwa na manufaa makubwa kwao watumiaji  wa serikali mtandao katika kukuza taaluma zao.

Amesema kuwa,wamejiwekea mikakati ya kuhakikisha wanaenda kutekeleza huduma ya serikali mtandao katika taasisi zao kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi wa taasisi zao.

“Kwa pamoja tumejiwekea mikakati ya kuhakikisha tunaenda kufanya vikao vyetu  kidigitali katika vikao mbalimbali ikiwemo vikao vya madiwani na kuondokana na matumizi ya makaratasi.”amesema.

Naye Mkurugenzi  wa Mamlaka ya serikali mtandao (eGA) ,Mhandisi Benedict Ndomba akielekezea maazimio waliyojiwekea amesema kuwa , kwa  pamoja wameweza kujiwekea  maazimio mbalimbali ikiwemo kuhakikisha taasisi za umma anatumia huduma ya serikali mtandao katika kuendesha shughuli zake pamoja na vikao vya madiwani ili kuweza kupunguza  matumizi ya makaratasi. 

Amesema kuwa,wamejiwekea maazimio ya kuhakikisha tovuti  zote zinaboreshwa  ili kuweza kwenda kisasa zaidi ,huku wakizitaka taasisi za umma kutoa  kipaumbele kwenye maswala ya Tehama .

Aidha amesema  kuwa,maazimio mengine ni pamoja na kuhakikisha wakuu wa taasisi za umma kuhakikisha wanasimamia kikamilifu usimamizi wa sheria za serikali mtandao, sambamba na kuiomba  serikali kuanzisha upekuzi kwa watumiaji wa huduma za Tehama. 

Kwa upande wake Naibu katibu mkuu ofisi ya Rais,menejimenti ya utumishi  wa umma na utawala  bora,Xavier  Daudi amesema kuwa, wanaenda kuyafanyia  kazi mapendekezo yote yaliyotolewa  katika kuhakikisha huduma ya serikali mtandao ina imarika zaidi. 

“Tunaendelea  kusisitiza zaidi matumizi ya Tehama kwani yatasaidia sana kuokoa gharama ya kutumia matumizi ya makaratasi huku tuhakikisha kunakuwepo  kwa matumizi  sahihi ya huduma mtandao. “amesema.

Tags

Chapisha Maoni

0Maoni
Chapisha Maoni (0)