Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akimkabidhi
zawadi ya picha ya Mlango unaopatikana Zanzibar Makamu wa Rais wa Benki ya
Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya Thomas Ostros mara baada ya Mazungumzo yao yaliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa
Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 23 Februari
2023.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akifanya
mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya Thomas
Ostros,
Mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius
Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 23 Februari 2023.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwa
katika picha ya pamoja Makamu wa Rais wa Benki ya Uwekezaji ya Umoja wa Ulaya
Thomas Ostros (kulia kwa Makamu wa Rais) pamoja na Ujumbe aliofuatana nao mara baada ya Mazungumzo
yao yaliofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa
wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam leo tarehe 23
Februari 2023.
Na Mwandishi Wetu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
Philip Mpango leo tarehe 23 Februari 2023 amekutana na kufanya
mazungumzo na Waziri wa Uchumi na Biashara za Kimataifa wa Ufaransa
Mheshimiwa Olivier Becht, Mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam.
Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amempongeza Waziri huyo kwa
ujio wake hapa nchini akiambatana na ujumbe wa wawekezaji na
wafanyabiashara 30 wanaoshiriki Jukwaa la Uwekezaji na Biashara baina ya
Tanzania na Umoja wa Ulaya. Amesema ujio wa ujumbe huo unaonesha
dhamira ya dhati ya Ufaransa ya kuimarisha uhusiano uliopo baina ya nchi
hizo mbili hususani katika sekta za uchumi.
Ameongeza kwamba Tanzania ina dhamira ya dhati ya kuimarisha mahusiano
yake ya kiuchumi na Ufaransa na milango iko wazi siku zote ili kushirikiana
katika njia zinazoweza kuendeleza uhusiano huo.
Makamu wa Rais amekaribisha ushirikiano wa kitaalamu kutoka Ufaransa
katika sekta ya uzalishaji mvinyo mkoani Dodoma ambapo zabibu hulimwa
kwa wingi kwa kuzingatia kwamba taifa la Ufaransa linasalia kuwa miongoni
mwa wazalishaji wa juu na wenye uzoefu mkubwa katika sekta hiyo. Pia
ameishukuru serikali ya Ufaransa kwa kuiunga mkono Tanzania kiufundi kwa
kutoa wataalam wake kufanya kazi na Mamlaka za Kitaifa za Tanzania
hususan katika sekta ya Uchumi wa Bluu Zanzibar.
Kwa upande wake Waziri wa Uchumi na Biashara za Kimataifa wa Ufaransa
Mheshimiwa Olivier Becht amesema Tanzania na Ufaransa zinaweza kuongeza
ushirikiano zaidi wa kiuchumi na uwekezaji hususani katika sekta ya Nishati
ikiwemo Nishati ya Jua na Nishati ya Upepo. Ameongeza kwamba ushirikiano
baina ya Ufaransa na Tanzania utachochea biashara na kuiwezesha Tanzania
kuhudumia vema nchi za Jirani kutoka na mazingira ya kijiographia iliopo.
Ameongeza kwamba serikali ya Ufaransa imeridhia uwepo wa usafiri wa moja
kwa moja wa ndege kutoka Paris hadi Dar es salaam utakaoanza mwezi juni
mwaka huu utakaoimarisha biashara na ushirikiano uliopo. Pia amaesema
muhimu kuweka mpangokazi utakaoainisha vipaumbele vya miradi mbalimbali
vya serikali na sekta binafsi kati ya Ufaransa na Tanzania kwani ipo fursa
kubwa ya kuwekeza pamoja na hicho ndicho Rais Emanuel Macron na Rais
Samia Suluhu Hassan wanachohitaji kwa sasa.
Katika hatua nyingine Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amekutana na
kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Benki ya Uwekezaji ya Umoja
wa Ulaya Thomas Ostros, mazungumzo yaliofanyika katika Ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam. Katika
Mazungumzo hayo wamejadili masuala mbalimbali ya ushirikiano baina ya
Tanzania na Benki hiyo hususani katika Miradi ya Maji, Bandari , Miundombinu pamoja na Nishati.